Saturday, February 9, 2013


TAHLISO: DAWA YA WANAVYUO MAKAHABA IPO JIKONI


UMOJA wa Serikali za Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) imekiri kuwapo kwa baadhi ya wanafunzi wa kike wanaotumia mitandao ya kijamii kufanya biashara ya ngono na kwamba ‘dawa yao ipo jikoni’

Akizungumza mjini Mtwara, Katibu Mtendaji wa TAHLISO, Donati Salla alisema kupitia uchunguzi wa awali uliofanya na umoja huo katika mitandano ya twitter, facebook, BBM na Instagram umebaini kuwapo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini pamoja na makundi ya mitandao ya wanafunzi hao.

Katibu huyo alikuwa alijibu habari ya kiuchunguzi iliyochapishwa na gazeti mwananchi wiki iliyopia, iliyobaini kuwapo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wanaotumia mitandano ya kijamii kufanya biashara ya ngono.

Februati 3 mwaka huu, gazeti hilo lilichapisha habari iliyopewa jina la Ripoti Maalum, ikiwa imebebwa na kicha cha habari “Wanafunzi wa kike vyuoni watumia mitandao kujiuza” ikiwataja baadhi ya wanafunzi wa kike wa Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Dodoma, SAUTI, Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Utawala wa Fedha (IFM) kuhusika na biashara hiyo.

“Sekretarieti imefanya uchunguzi wa awali juu ya uwapo wa mitandano na mtandao wa makundi ya wanafunzi wanaojishughulisha na ukahaba….tulifanikiwa kuwakuta katika mitandao iliyotajwa…TAHLISO sasa itafanya uchunguzi wa kina ili kupina ukweli wa taarifa hizi” alisema Salla na kuongeza

“Wale tutakaowakamata wakifanya vitendo hivyo vya aibu taarifa zitapelekwa katika vyuo vyao kwa hatua zaidi, uongozi wa TAHLISO utaangalia njia sahihi za kukabiliana na tatizo hili ikibidi njia za kisheria…pia nawaomba viongozi wa jumuiya za kidini za wanafunzi na vyuo kuchunguza katika maeneo yao na kubaini njia sahihi kukabiliana na tatizo hili ambalo linaharibu heshima ya vyuo vikuu nchini”

No comments: