MFANYABISHARA AKUTWA NA JENEZA SOKONI
MWENYEKITI wa wafanyabiashara katika soko Kuu jijini Mwanza, Hamad Nchola amekamatwa na jeneza aliloficha chini ya magunia ya viazi katika biashara yake.
Nchola ambaye ni mfanyabiashara sokoni hapo aliwashangaza wafanyabiashara wenzake kwa kitendo cha kukutwa na jeneza hilo katika bidhaa anazouza.
Nchola aliweka jeneza hilo katikati ya magunia ya viazi mbatata ambayo alikuwa anayauza sokoni hapo.
Jeneza hilo lilionekana katika wakati wa pilikapilika za sokoni na kuwafanya wafanyabiashara kuanza kumlalamikia kwa kitendo hicho licha ya kuwa yeye ni kiongozi sokoni hapo.
Wafanyabiashara hao walimtaka kiongozi wao huyo atoe ufafanuzi kwanini aliweka jeneza hilo hapo lakini hakuonesha ushirikiano kwa kutoa majibu yasiyoridhisha kwa wenzake.
Wafanyabiashara hao walidiriki kulibeba jeneza hilo juujuuu na kudai watamfungulia, mashitaka na kumlalamikia kwa kuwadhalilisha kwa wateja kwa kitendo hicho alichofanya.
Hata hivyo kuna baadhi ya wafanyabishara walikiona kitendo hicho na kukihisi kuwa ni cha vitendo vya ushirikina.
Nchola alipoulizwa na wenzake ni kwanini aliweka jeneza hilo alijibu “Kama kuweka jeneza nimeweka kwenye biashara yangu kwani lipi la kustaajabisha mimi nimehifadhi na ninyi haiwahusu" alijibu
No comments:
Post a Comment