Sunday, February 3, 2013

GHANA NA MALI ZATINGA NUFU FAINALI AFCON



Ghana ilikuwa timu ya kwanza kuingia nusu fainali ya michuano ya AFCON baada ya kuicharaza Cape Verde 2-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali.

Ghana imepata bao la kwanza katika kipindi cha pili likifungwa na Mubarak Wakaso kwa njia ya penalti katika dakika ya 54.

Wakaso tena iliihakikishia Ghana kusonga mbele baada ya kufunga bao la pili katika dakika ya tisini.

Kwa matokeo hayo Cape Verde imeyaaga rasmi mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Hata hivyo Cape Verde ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza ilionyesha upinzani mkubwa na michuano hiyo inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Mchezo kati ya Ghana na Cape Verde ulifanyika mjini Port Elizabet

Mechi nyingine ilizikutanisha wenyeji wa michuano hii, Afrika Kusini kwa kupambana na Mali mjini Durban. Hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Goli la Afrika Kusini limefungwa katika dakika ya 31 na Tokelo Rantie.

Hata hivyo Mali ilisawazisha goli hilo katika dakika ya 58 kipindi cha pili likifungwa na Seydou Keita.

Hata hivyo baada ya kuongeza dk 30 mambo yakawa bila bila.

Ndipo hatua ya matuta ikafuatiwa ambapo mali waliweza kupata penalti 3 dhidi ya moja ya afrika ya kusini.

Robo fainali nyingine itapigwa leo kati ya Ivory Coast na Nigeria

Bukina faso wakivaana na Togo

No comments: