INTER MILAN YATOZWA FAINI KWA VITENDO VYA UBAGUZI
KAMATI ya nidhamu ya
Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A limeitoza faini ya euro
50,000 klabu ya Inter Milan baada ya mashabiki wake kukutwa na hatia ya
kumfanyia vitendo vya kibaguzi mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo
Mario Balotelli. Tukio
lilitokea wakati Balotelli akiichezea kabla yake mpya ya AC Milan
katika mchezo dhidi ya Inter ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao
1-1. Mashabiki
wa Inter walikuwa wakipeperusha maganda ya ndizi katika mchezo huo
lakini baadhi wachambuzi walidai pengine tukio hilo halikumlenga nyota
huyo ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka minne. Balotelli
ambaye ametokea Manchester City kabla ya kwenda AC Milan naye pia
metozwa euro 10,000 kwa kuwaonyesha ishara ya matusi mashabiki hao
No comments:
Post a Comment