Thursday, January 24, 2013


Refa Chris Foy akimtoa Hazard kwa kadi nyekundu
SWANSEA City wametinga katika fainali yao ya kwanza ya Kombe la Ligi baada ya kuwashikilia Chelsea waliobaki 10 uwanjani katika sare ya bila goli kwenye nusu fainali ya utata katika Uwanja wa Liberty Stadium.
Matokea ya jumla yaliwapa Swansea ushindi wa 2-0, lakini yalisaidiwa kidogo mno na kutolewa na kwa kadi nyekundu kwa kiungo wa Chelsea, Eden Hazard ambaye alimpiga teke mtoto anayeokota mipira.

Kiungo huyo Mbelgiji alitolewa katika dakika ya 80 baada ya kutukio hilo lililotokea nyuma ya goli la wenyeji.
Swansea sasa watacheza dhidi ya timu ya daraja la nne ya Bradford katika fainali kwenye Uwanja wa Wembley.
Kadi nyekundu ya Hazard ilikuja baada ya kuvutana na muokota mipira, ambaye alikuwa akichelewa kurejesha mipira ukwa kitendo hicho, baadaye aliiambia Chelsea TV: "Kijana aliweka mwili wake wote juu ya mpira na mimi nilikuwa najaribu kuupiga mpira.

"Nadhani nilipiga mpira na si mvulana. Naomba radhi."


Polisi wa Wales Kusini walisema watachunguza tukio hilo, ambalo lilitokea wakati mpira ulipotoka kwa ajili ya kupigwa "goal kick" katika dakika ya 80.

Meneja wa habari wa Swansea City, Jonathan Wilshere alisema: "Polisi wamemhoji kijana, ambaye jina lake halitajwi kwa sababu umri wake ni chini ya miaka 18.

"Yeye na baba yake walizungumza na polisi na hawafungui mashitaka. Alikuwa kwenye chumba cha kuvalia cha Chelsea na alipeana mikono na Hazard. John Terry na Frank Lampard walimkaribisha vyema kwenye chumba cha kuvalia cha Chelsea."

Kocha wa Chelsea, Rafael Benitez alisema wote wawili, mchezaji na kijana waliombana radhi baada ya mechi hiyo kwenye Uwanja wa Liberty.

Aliongeza: "Wote wamebaini walikuwa na makosa.

"Mvulana aliomba radhi kwa kupoteza muda. Hazard alikuwa amefadhaika na akawa anajaribu kuupata mpira. Aliupiga mpira na akaupata.

"Tunaweza kulichunguza tukio kwa nusu saa lakini sote tunajua kwamba wote walikuwa na makosa.

"Tunalishughulikia ndani, hicho ndicho ninachoweza kusema."

Refa wa zamani wa Ligi Kuu ya England, Dermot Gallagher aliiambia BBC Radio 5 live: "Kulikuwa na adhabu wakati beki wa Liverpool, Jamie Carragher alipotolewa kwa kadi nyekundu baada ya kurusha sarafu kuelekea kwa mashabiki dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Highbury mwaka 2002.

"Refa Chris Foy alikuwa sahihi kabisa kumtoa Eden Hazard, ni tukio lisilokubalika. Alikuwa sahihi kabisa kumtoa. Ataripoti suala hilo kwa chama cha soka (FA)." wanjani. Alionekana kuulalia mpira na picha za TV zilionyesha Hazard akimpiga teke.

No comments: