IVORY COAST YAINGIA HATUA YA MTOANO YAIKANDAMIZA TUNISIA 3-0
TOGO NAYO YAIGAGADUA ALGERIA MABAO 2-0
Timu Ivory Coast imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya mtoano ya michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuisambaratisha Tunisia kwa magoli 3-0 katika mechi yao ya Kundi D katika michuano ya AFCON nchini Afrika Kusini.
Winga wa Arsenal, Gervais Kouassi a.k.a Gervinho aliipatia Ivory Coast goli la kuongoza kwa chuti lililotinga kwenye dari baada ya kugongeana na mshambuliaji wa Anzhi Mckhachkala, Lacina Traore, ambaye alimrejeshea mpira kwa pasi ya kisigino katika dakika ya 21.
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure, alithibitisha sifa yake barani hapa baada ya kufunga goli kali la pili kwa shuti la kutokea nje ya boksi lililoenda kutinga kwenye nyavu ndogo katika dakika ya 85, kabla ya Didier Yakonan kuhitimisha ushindi mnono wa kujiamini katika dakika ya 88.
Ushindi unamaanisha kwamba Ivory Coast imetinga katika hatua ya mtoano baada ya kufikisha pointi sita. Ivory Coast imefunga magoli matano na kufungwa goli moja.
Katika mchezo mwingine timu ya Togo imeifunga Algeria mabao 2-1, mabao yaliyofunga na Emanuel Adebayo Dk ya 31 ya mchezo huku bao la pili likishindiliwa na Dove Wome ambaye alitokea benchi.
Togo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu sawa na tunisia lakini togo ikiwa na mabao 2.
Michuano hiyo inaendelea kesho kwa kundi C, ambapo mechi ya kwanza itawakutanisha Morocco na wenyeji Afrika ya kusini wakati mechi ya pili ni kati ya Cape Verde na Angola
No comments:
Post a Comment