UGANDA BINGWA MICHUANO YA CECAFA, ZANZIBAR YASHIKA NAFASI YA 3
![]() |
Kikosi cha timu ya Uganda The cranes |
UGANDA The Cranes imetwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge jioni ya leo, Kwa mara 13 baada ya kuibanjua Kenya, Harambee Stars mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Mandela uliopo Namboole mjini Kamapala Uganda
Mchezo huo, ulitanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu, kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Zanzibar ilishinda kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, Bara wakitangulia kupata bao kupitia kwa Mwinyi Kazimoto dakika ya 10 kabla ya Abdallah Othman Ali kuisawazishia Zanzibar dakika ya 85
No comments:
Post a Comment