Monday, December 10, 2012

AJIUA KWA MATAMANIO YA NGONO YA MARA KWA MARA
Gretchen Molanen wakati wa uhai wake
Mwanamke mmoja nchini ufaransa aliyefahamika kwa jina la Gretchen Molanen (23) amechukua uwamuzi wa kujiua kwa sababu ya kusumbulia na ugonjwa wa ajabu unaomfanya atamani kufanya mapenzi mara kwa mara bila ya kuishiwa hamu ya tendo.
Ungonjwa huo unaofahamika kwa jina la (female sexual arousal disorder) unazichochea sehemu za siri kutamani kufanya mapenzi mara kwa mara bila ya kuisha hamu.

Imeelezwa kwamba ugonjwa huo hatari unawapata wanawake tu, kulingana na mtandao mmoja wa kifaransa , unamfanya mwanamke kutamani kufanya ngono wakati wote, bila ya kujali nani anafanya naye tendo hilo, na hakuna kitu kinachoweza kupunguza mataanio hayo mpaka pale hisia hizo zitakapopungua wenyewe, hali hiyo hudumu kwa muda wa masaa kadhaa mpaka siku mzima.

Wanasayansi wamesema kwamba ugonjwa huo ni matokeo ya udhaifu na ulegevu wa mishipa ya sehemu za siri za mwanamke, na wala hauna mahusiano na matamanio ya kufanya ngono kwa kuvutiwa kimapenzi, Gretchen aliacha kazi ili apate muda wakutosha kujitibia lakini baada ya kuona hakuna ufumbuzi wa tatizo lake aliamua kujiua.

No comments: