Tuesday, December 4, 2012

MWANAMKE AJIKUTA AKIVUA NGUO KWENYE SHUGHULI BAADA YA KUFAKAMIA POMBE, MUME ATANGAZA KUTOA TALAKA

MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Mamuu [30] mkazi wa Yombo Vituka jumamosi iliyopita aliitia aibu familia yake baada ya kufakamia kinywaji aina ya bia na kujikuta akifanya vioja hali iliyofanya mume kucharuka na kutangaza kutoa talaka kuhusiana aibu aliyo.
MWanamke huyo mama wa watoto wawili imedaiwa si mzoefu a kinywaji hicho bali siku hiyo kwenye mkesha wa sherehe ya harusi ya mtoto ya jirani yake bila kutambua athari ya kinywaji hicho majira ya saa 11 jioni akiongozana na ndugu wa
 karibu wa wenye sherehe hiyo kupata kinywaji hicho ili waweze kusherehesha vizuri sherehe hiyo ambayo ilipaniwa na wa wanawake hao.

Imedaiwa kuwa wakati wanakwenda kupata kinywaji hicho moja ya ‘grosari’ iliyo karibu na mtaa wanaoishi ndugu hao walijua jirani huyo huenda alikuwa mzoefu katika masuala bila kutambua mwenzao si mzoefu katika kubugia kinywaji hicho.

Imedaiwa kwa kuwa walikuwa na furaha kubwa Mwenyezi Mungu kuwafikisha siku hiyo mbayo waliipania walianza kinywaji hicho na wmanamke huyo alipomaliza kinywaji hicho alidai aongezwe cha pili na mara baada ya kumaliza hicho ilidaiwa aliongeza cha chupa ya tatu ambayo ndiyo ilimfanya aadhirike na kupatwa na aibu hiyo kubwa

Imedaiwa kuwa, mara baada ya kumaliza kinyaji hicho hali ya mwanamke huyo ilianza kubadilika wka kuanza kuropoka huko na huko, kuanza kutukana matusi ya nguoni kwa kila amuonae mbele yake hali iliyozua mtafaruku na wenzake hao wakaamua wamsitishie kinywaji na kumshi akampumnzike kwani hakuweza kuhimili vishindo

Hata hivyo mwanamke huyo hakuwa tayari kurudi nyumbani na  usiku ulishaingia na maajabu makubwa yalionekana zaidi wakati wa uchezaji mziki akaonekana akivua nguo kwa kuwa fahamu zilimtoka kwa pombe jambo lilofanya wenye shughuli kumbeba na kumpeleka ndani akapumzike

Hata hivyo haikuwa dawa baada ya dakika kadhaa mwanamke huyo katikati ya mziki wakati akicheza alijikuta akianza kusaula nguo moja baada ya nyingine ndipo hapo baadhi ya wenye shughuli waliamua wamfungie katika moja ya chumba ili kumsitiri aibu anayofanya

Hivyo wakati yote hayo yakiendelea mume wa mwanamke huyo alikuwa bado hajafika nyumbani kwake na alipofika nyumbani kwake majira ya saa 3 usiku baadhi ya majirani mashuhuda walimtonya mambo aliyokuwa akifanya mke wake katika shughuli hiyo ndipo mume huyo kwa hasira akathibitisha mke wake kufungiwa katika moja ya chumba na kwa aibu hiyo aliyodai ni kubwa kwake alitangaza kumpa talaka mwanamke huyo kwa kuwa aibu hiyo hajui pa kuificha


Hata hivyo imedaiwa na mmoja wa majirani siku iliyofuata baada ya mwanamke huyo pombe kumuishia aliadiiwa aliyoyafanya na alimtaka radhi mume wake huyo lakini mume huyo tayari alishakuwa katika adhimio la kuandika talaka ampatie mke wake huyo kutokana na aibu kubwa alioyompatia mtaani.


Chanzo; nifahamishe.com 
 

No comments: