AFCON 2015: EQUATORIAL
GUINEA NA CONGO ZASONGA MBELE ROBO FAINALI
Wenyeji Equitoria Guinea na Congo Brazaville zimekuwa timu za kwanza kusonga mbele katika hatua ya robo fainali kutoka kundi A ya Michuano ya Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada timu hizo shindi mechi zao hapo jana usiku.
Equitoria
Guinea iliwaadhibu wapinzani wao Gabon kwa jumla ya magoli 2 bila majibu, huku
Congo Brazaville nayo ikiwashushia kipigo Burkina Faso cha magoli mawili kwa
moja.
Wenyeji
Equitorial Guinea waliandika bao la kwanza katika dakika ya 55 kipindi cha pili
kwa mkwaju wa penalti baada ya Lloyd Palun kufanyiwa faulo katika eneo la
hatari.
Kama
hiyo hatoshi Wenyeji hao wakapigilia msumari wa moto kwenye kidonda pale
waliondika bao la pili kupitia Salvador Iban ambaye aliukwamisha mpira wavuni
uliotemwa na mlinda mlango wa Gabon.
Nayo
Congo Brazavile ambayo ilihitaji sare ya aina yoyote ili isonge mbelehatua ya
robo fainali ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa mchezaji Thierry Bifouma
huku goli la pili likifungwa na Fabrice Ondama.
Goli
pekee la Burkina Faso lilitiwa wavuni na Aristide Bance.
Kwa
matokeo hayo Congo Brazaville inaingia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza
ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa mara kwanza tangu mwaka 1992.
Leo
kutakuwa na mechi mbili za kundi B ambapo timu mbili kutoka ukanda wa Afrika
Mashariki na kati Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia zitatupa karata
zao za mwisho ambapo Jamuhuri Kidemokrasia ya Kongo itaumana vikali na Tunisia
huku Zambia ikikutana uso kwa uso na Cape Verde.
Zambia
na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lazima zishinde mechi zao leo ili ziweze
kusonga mbele hatua robo fainali huku Zambia ikihitaji ushindi wa magoli zaidi
ya matatu kwa bila.
MSIMAMO-Makundi B hadi D
No comments:
Post a Comment