Tuesday, October 7, 2014

PAPA MTAKATIFU KUJADILI NDOA NA TALAKA KANISANI

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amefungua rasmi mkutano wa viongozi wakuu wa kanisa hilo kujadili maswala kama vile uzazi wa mpango, talaka na ndoa za jinsia moja.
Wanaojadili maswala haya ni viongozi wa kanisa hilo na wanatarajiwa kufanya hivyo kwa uwazi bila uoga wowote.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya Vatican, David Willey anasema kuwa Papa alifungua mkutano huo na kuwataka viongozi hao kuongea bila uoga wowote kwa kipindi cha wiki moja.
Papa alianzisha mjadala wa baadhi ya mambo ambayo ni mwiko kwa wengi wa viongozi wa kanisa na kuwataka kuyajadili bila uoga.
Aliwaambia zaidi ya viongozi 200 wa kanisa hilo pamoja na wataalamu kuongea bila hofu ya kumuudhi, kuongea ukweli na kwa uwazi na kusikiliza kwa umakini. Mkutano huu ni wa kipekee kwani mikutano ya Vatican kwa kawaida huwa na kimya kingi.
Lugha ambayo hutumika kwa kwaida huwa imejaa maneno yanayoambatana tu na mafunzo ya kanisa.
Papa Francis alifungua rasmi mkutano huo na kuwataka viongozi wengine kuongea kwa uwazi. Papa amekuwa akitaka gumzo katika kanisa kuhusiana na maswala ya ngono na pengo lililopo katika mafunzo ya dini na masuala kuhusu familia na ambavyo familia za kikatoliki zinaishi maisha yao.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala kuhusu ikiwa ni sawa kuruhusu wakatoliki wanaotalakiana na kisha kuona tena kukubaliwa kupokea sacramenti.
Papa Francis anataka kanisa kuwaonea huruma watu waliotalakiwa bila ya kulegeza msimamo kuhusu maswala ya ndoa.
BBC Swahili

No comments: