WACHUNGUZI KUKUTANA NA MAAFISA WA FIFA KUHUSIANA NA TUHUMA ZA RUSHWA QATAR.
Waandalizi
wa kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar wanatarajiwa kukutana na mchunguzi wa
shirikisho la soka duniani FIFA, Michael Garcia hii leo huku kukiwepo wito kwa
taifa hilo kunyimwa haki ya kuandaa mashindano hayo.
Jumapili,
gazeti la SUNDAY TIMES la Uingereza, liliripoti kwamba mamilioni ya pauni
zilitolewa kama malipo kwa maafisa waliounga mkono ombi la Qatar kuandaa
michuano hiyo mwaka 2022, tuhuma ambazo Qatar imepinga vikali.
Fifa
imesema ombi jipya linapaswa kuruhusiwa iwapo tuhuma hizo za rushwa
zitathibitishwa. Makamu wa Rais wa Fifa, Jim Boyce, anasema kuwa ataunga mkono
hatua ya kupiga kura tena ikiwa madai hayo yatathibitishwa ili kuteua nchi
nyingine.
Bin
Hammam afisa wa soka Qatar ndiye anadaiwa kuwalipa hongo maafisa wa FIFA.
Afisaa
mmoja wa kamati ya FIFA, Lord Goldsmith, alisema kuwa ''Ikiwa itathibitishwa
kuwa uamuzi wa kuipa Qatar idhini ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022
ulitokana na hongo kulipwa maafisa wa shirikisho la FIFA, basi uamuzi wa
kuinyima nchi hiyo haki hiyo lazima uchukuliwe. ''
Aliyekuwa
mkurugenzi mkuu wa FA Mark Palios, anadhani kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter
anajitahidi kulinda kazi yake.
Garcia
anatarajiwa kukutana na maafisa wa FIFA nchini Qatar. Wakili huyo anachunguza
madai mengine ya tuhumza dhidi ya maafisa wa FIFA kuhusiana na kombe la dunia
mwaka 2018 na 2022.
Jarida
la Sunday Times, linadai kuwa maafisa wa soka walipokea hongo ya kima cha pauni
milioni 3 ili waweze kuunga mkono azma ya Qatar kutaka kuandaa kombe la dunia
mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment