GHANA YATUHUMIWA KWA UFISADI
KOMBE LA DUNIA, FIFA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UBAGUZI KWA MASHABIKI WA UJERUMANI
Kikosi cha Ghana |
Shirikisho
la soka nchini Ghana limewataka maafisa wa polisi kuingilia kati baada ya madai
ya vyombo vya habari vya Uingereza kwamba mmoja wa maafisa wake alikubali timu
ya nchi hiyo kucheza katika mechi zilizo fanyiwa ufisadi.
Madai hayo yametolewa kufuatia uchunguzi wa pamoja kati ya gazeti la Uingereza la Daily Telegraph na Runinga ya Channel Four.
Katika taarifa yake shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa hakuna ushahidi kwamba uadilifu wa michuano ya kombe la dunia umeathirika.
Shirikisho la soka nchini Ghana limesema kuwa litamuekea vikwazo vikali afisa yeyote atakayepatikana na makosa hayo.
WAKATI HUOHUO SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA linatarajia
kuchunguza tuhuma za ubaguzi zinazodaiwa kutolewa na mashabiki wa Ujerumani
katika mchezo dhidi ya Ghana ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 huko
Fortaleza.
Picha zilionyesha baadhi ya
mashabiki wakiwa wamejipaka rangi nyeusi katika nyuso zao katika mitandao ya
kijamii, na kuzua mjadala kuwa mashabiki wa timu za Ulaya wanaonyesha tabia za
kibaguzi. Kuongezea uzito madai hayo ni tukio la mshabiki mmoja, ambaye
aliingia uwanjani akiwa na maandishi kuhusu Nazi wakati wa kipindi cha pili cha
mchezo huo. Msemaji wa FIFA amesema siku zote wanachukua ushahidi wowote
unaowasilishwa au kuonekana katika kamati yao ya nidhamu na wao ndio
wanaokutana kuangalia kama wanaweza kufungua kesi na baadae tume ya nidhamu
kutoa maamuzi.
No comments:
Post a Comment