Tuesday, May 27, 2014

IJUE NDOA ILIYODUMU KWA SIKU 13 TU.

Bonface Oduor na Sarah Kayuga siku ya harusi yao
Inaweza kuingia kwenye rekodi kama ikizihusisha ndoa zilizodumu kwa muda mfupi tena zikifungwa kwa baraka zote kuanzia kwa wazazi hadi kwa Mungu kulingana na sehemu ilikofungwa ndoa hii ambapo ilikua kanisani.
Bonface Oduor ambaye ndiye bwana harusi amesema  ‘Alinisaliti baada ya siku 13 ya harusi yetu ilofanyika wikendi ya pasaka’.
Wasiwasi na Uwoga mkubwa wa Bonface Oduor ilitimia hivi maajuzi tu baada ya kumfumania mkewe akishiriki tendo la ndoa na mwanaume mwingine ikiwa ni siku 13 tu baada ya harusi yao.
Jamaa ambaye alimfumania mkewe aitwae Sarah Kayuga kwenye hotel moja ya hotel za Nairobi akiwa na mwanamume  mwingine.
Harusi yao ya kufana ilifungwa kwenye kanisa la Pentecostal Assemblies of God Diani Mombasa  Aprili 13 ambapo Oduor amedai ilikua ni ya kupoteza muda na pesa na akaapa kutoishi tena na mwanamke na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi tena kwani hana imani tena na wanawake.
Hata hivyo Wawili hao waliamua kuachana baada ya oduor kugundua kua sarah alikua ametupa picha zake kwenye mtandao wa wozzup akiwa uchi.

No comments: