UKISTAAJABU
YA MUSA UTASHANGAA YA FILAUNI, MWANAMKE ALIYEOLEWA ANAISHI NA MUME NA BOYFRIEND
NYUMBA MOJA
![]() |
|
Maria Butzki na wapenzi wake, Maria akiwa na
mumewe Paul (kushoto) na boyfriend Pater (kulia)
|
Tumezoea kuona au kusikia zaidi
mwanaume kuwa na uhusiano na wasichana wawili ambao wanajifahamu, lakini huko
Uingereza mwanamke mmoja ameamua kuishi na wanaume wake wawili nyumba moja,
mmoja ni mume wake wa ndoa na mwingine ni boyfriend wake
Mwanamke huyo Maria Butziki (33)
mama wa watoto wawili anauita uamuzi huo kuwa ni perfect solution ya tatizo
lililokuwa linamtatiza la kushindwa kumuacha yeyote kati yao sababu anawapenda
wote.
Cha kushangaza zaidi ni kuwa wanaume
wote wawili wamekubaliana na uamuzi huo na wanaishi kwa furaha kama familia
moja pamoja na watoto wawili wa Maria. Maria aliwahi kuachana na mumewe Paul na
kuanzisha uhusiano na Peter kabla hajagundua kuwa moyo wake hauwezi kumsahau
mumewe na wakati huo huo hawezi kumuacha Peter.
Upande wa mumewe Paul yeye kamsifia
mume mwenza kuwa ni mkt makini.
Upande wa Peter naye amesema
anaelewana vizuri na mume wa mpenzi wake na wala haoni wivu kushirikiana naye
mpenzi .
Pamoja na kuwa wana mahusiano ya
kimapenzi lakini Maria amesema huwa hajichanganyi nao chumba kimoja, boyfriend
hulala kwenye kochi wakati mume ana chumba chake na Maria hulala na mtoto wake
mkubwa wa kike.
Najua unaweza kuwa unajiuliza
watatu hawa wanautaratibu upi katika swala la kushiriki tendo la ndoa, Maria
amesema mmoja kati yao anapokuwa ametoka basi aliyebaki ndio anapata nafasi ya
kufanya naye mapenzi lakini hawajawahi kuzungumza kwa pamoja kuhusu swala hilo.

No comments:
Post a Comment