AFIKISHWA
MAHAKAMNI KWA KUIBA PETE YA UCHUMBA YA RAFIKI YAKE NA KUMVALISHA MPENZI WAKE.
Kijana mmoja
kutoka eneo la Korogocho Nairobi nchini Kenya amefikishwa mahakamani
kwa tuhuma za kuiba pete ya ndoa ya rafiki yake na kumvesha mchumba wake.
Ahmed Abdirahman,27 anatuhumiwa kuiba pete hiyo ya dhahabu yenye
thamani ya Sh35, 000 za Kenya kutoka
kwa Kadar Mohammed siku ya May 23 huko
Korogocho Nairobi nchini Kenya na baadaye kumvesha mchumba wake
kwa madai kwamba amenunua kwa ajili yeke.
Kadar aliiambia mahakama kwamba walikuwa pamoja na Ahamad ambaye ni
rafiki yake mkubwa katika mradi unaojishughulisha na vijana ndipo ahamad
alipofanya tukio hilo.
Na alipojaribu kuumuuliza rafiki yake kama aliiona pete hiyo lakini Ahamad
alikataa katakata kuiona pete hiyo.
Ilimbidi awashirikishe na
wazazi wake juu ya tukio hilo lakini aliendelea kukataa kwamba ajaiba pete
hiyo.
Baadaye aliiona pete hiyo ikiwa imezaliwa na mchumba wa rafiki yake, yaani
mpenzi wa Ahamad ndipo alipokwenda kuripoti police na kumsweka korokoroni.
Hata hivyo Ahamad alikataa mahakani mbele ya hakimu Emilly ominde na kuachiwa kwa dhamana ya Sh.
10,000 mpaka kesi iatakaposikilizwa tena mwezi ujao.
Daily post
No comments:
Post a Comment