TFF YATEUA WAKILI WA KUCHUNGUZA USAJILI WA DOMAYO
Kutokana na tukio lililotokea jana (Aprili 30
mwaka huu) kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani
Mbeya likihusisha usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo
mzima wa tukio hilo.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili
Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau
wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
Domayo amesajiliwa na Azam FC akiwa kambini
Taifa Stars mjini Tukuyu wakati timu hiyo inajiandaa kucheza mechi ya kirafiki
dhidi ya Malawi.
Usajili wake umezua gumzo huku TFF ikiendelea
kusisitiza kwenye kambi za timu ya taifa si sehemu sahihi ya kufanya masuala ya
usajili.
No comments:
Post a Comment