Sunday, April 27, 2014

HATIMAYE TIMU YA CHANG’OMBE FC YA NDUMBWE YATAWAZWA MABINGWA WAPYA WA LIGI DARAJA LA NNE MTWARA VIJIJINI
Chang’ombe FC mabingwa wapya Mtwara vijijini
New stars


   Mashabiki wa chang'ombe wakifurahiya ushindi wa timu yao
Katibu wa chama soka Mtwara vijijini Selemai Samkwa kushoto akiwa na Ally Kumbo kulia wakifuatilia mechi
Sospiter Magumba kushoto na Samkwa
Mbuke Rashidi mchambuzi wa soka Pride Fm Radio naye alikuwepo
Nalinga Ally Faki akiingia uwanjani
 Timu ya Chang’ombe FC ya  Ndumbwe  Mtwara vijijini leo hii imeibuka bingwa wa ligi daraja la nne mtwara vijijini baada ya kuisambaratisha New stars ya Mbawala kwa mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Nagwanda Sijaona Mjini Mtwara.

Mchezo wa huo ulivuta hisia za mashabiki wengi wa mtwara mjini na vijijini kutokana na sakata la mchezaji Nalinga Ally Faki wa timu ya New Stars ambaye alizua sintofahamu ndani ya uongozi wa chama cha soka mtwara vijijini MRDFA baada ya mchezaji huyo kufungiwa mwaka mmoja kutocheza mpira wa miguu baada ya kubainika kwamba alisajili timu mbili.

Lakini baadaye alifunguliwa na kamati ya nidhamu ambayo haikufahamika kamati hiyo inaongozwa na nani, kabla ya adhabu yake kumalizika. Jambo ambalo lilizua mgogoro baina ya viongozi wa chama hicho na hatimaye mwenyekiti wa chama hicho Rashidi Chande kuingilia kati na kutengua matokeo ya mchezo nusu fainali ya kwanza kati ya Shivo na New Stars ambao new stars ilishinda bao 1-0 na kuwapa shivo pointi tatu na magoli 3 baada ya new stars kubainika kumchezesha mchezaji Nalinga Faki kinyume na taratibu. Na katika fainali ya pili new stars walifungwa mabao 3-1 hivyo kuwapa tiketi shivo kucheza fainali kutokana na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Hatimaye mgogoro huo uliendelea kufukuta na kusuluhishwa na kamati ya nidhamu na haki za wachezaji ya chama cha soka Mkoani Mtwara  MTWAREFA baada ya new stars kukata rufaa na kushinda kucheza fainali na Chang’ombe.

Kwa mtokeo hayo timu za Chang’ombe Ndumbwe,  New Stars na Chimbuko za mbawala juu zimepata tiketi za kucheza ligi ya mkoa.

No comments: