DUNIANI KUNA MAMBO: AJARIBU KUJIZIKA HAI KUKWEPA MATATIZO YA NDOA
Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha
wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya
kujichimbia kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni
matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu
wa kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne
asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift ValleyMwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndio maana akaamua kujitoa uhai.
Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumbwa na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.
No comments:
Post a Comment