Thursday, March 20, 2014

UEFA CHAMPIONZ LIGI, VAN PERSIE AIPELEKA MAN UTD ROBO FAINALI
Mabao matatu yaani HETITRIKI ya Robin van Persie Usiku wa kuamkia leo huu imewapa Manchester United ushindi wa Bao 3-0 dhidi ya Olympiakos na kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Jumla ya Bao 3-2 katika Mechi mbili.

Hadi Mapumziko, Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-0, la kwanza likiwa kwa Penati baada ya Van Persie kufanyiwa Faulo.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Mabingwa hao wa England hasa ukizingatia walikuwa wamefungwa 2-0 katika Mechi ya Kwanza na pia Jumapili walichapwa na Liverpool Bao 3-0 na kila Mtu alikuwa akimsakama Meneja David Moyes kwamba hana jipya.

DORTMUND 1 ZENIT 2
Wakicheza kwao Signal Iguna Park huko Jijini Dortmund, Germany, Borussia Dortmund Usiku wa kuamkia leo wamechapwa Bao 2-1 na Klabu ya Urusi, Zenit St. Petersburg ya Urusi lakini wamefuzu kuingia Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Jumla ya Bao 5-4.
Dortmund waliifunga Zenit Bao 4-2 huko Urusi katika Mechi ya Kwanza.
Bao za Zenit zilifungwa na Givaldinho Hulk, Dakika ya 16, na Jose Salomon Rondon, Dakika ya 73 wakati Bao la Dortmund Mfungaji alikuwa Sebastian Kehl katika Dakika ya 39.

TIMU ZILIZOTINGA ROBO FAINALI:

-Bayern Munich

-Atletico Madrid

-Barcelona

-Paris Saint-Germain

-Chelsea

-Real Madrid

-Manchester United

-Borussia Dortmund

No comments: