DUNIANI
KUNAVITUKO,MWANAMUME AMTOA MKEWE KAMA MALIPO YA DENI
![]() |
Moi’s Bridge, |
MWANAMUME
katika kijiji cha Lwanda, kata ndogo ya Moi’s Bridge, katika jimbo ndogo la
Likuyani nchini Kenya ameshangaza wakazi baada ya kukataa kulipa deni la Sh900
na badala yake akamtoa mkewe kama malipo.
Kwa
mujibu wa Patrick Andabwa, aliyekuwa akidai deni lake, alimsaidia mwanamume
huyo kutengeneza matofali. Hata hivyo baada yake kumaliza kazi,alikataa kumlipa
pesa zake na badala yake akamwambia amchukue mkewe.
Ingawa
mimi bado ni kapera, nimeamua kumchukua na siangalii nyuma,” akasema mwanamume
huyo wa umri wa miaka 22.
Mwanamke
mhusika aliyetambuliwa kwa jina Jones Kevogo hakupinga mpango huo.
Alisema
alikubali kwa sababu mumewe alikuwa na mazoea ya kuajiri wafanyakazi na kisha
kukataa kuwalipa akidai kwamba walikuwa wameanzisha uhusiano wa kimapenzi naye.
“Hii
si mara ya kwanza,” akasema na kuongeza kuwa mwanamume huyo ametumia ‘mbinu’
hiyo mara kadha kukwepa kulipa madeni ya watu.
Jones,43,
ambaye ni mama wa watoto watano alisema ameamua kuachana na aibu ya kuhusishwa
na mumewe ambaye wameishi pamoja kwa miaka 20.
“Nina matumaini kwamba ndoa yangu mpya
itafanya kazi licha ya tofauti kubwa ya kiumri kati yetu,” akasema akidai
kwamba alikuwa akidhulumiwa katika ndoa yake ya awali.
Alisema
hatabadilisha uamuzi wake wa kumuacha mumewe hataka kama ndoa yake ya sasa
itasambaratika. Alieleza kuwa watoto waliowazaa na mumewe wako huru
kumtembelea.
No comments:
Post a Comment