UTAMADUNI NA MICHEZO.
Mbunge
wa Kondoa Kusini (CCM) Juma Mkamia ametangazwa kuwa Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo.
Nkamia
anachukua nafasi ya Amos Makala ambaye amehamia katika wizara nyingine ya maji.
Nkamia
aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Simba, ametangazwa leo wakati wa baraza jipya
la mawaziri ambalo limetangazwa baada ya baadhi ya mawaziri kufutwa kazi na
wengine kujiuzuru.
Nkamia
ambaye taaluma yake ni mwandishi wa habari amewahi kufanya kazi ya utangazaji
katika mashirika mbalimbali likiwemo Redio Tanzania, TBC na yale ya kimataifa
kama BBC na Voice of America (VOA).
No comments:
Post a Comment