MECHI ZA FAINALI NA MSHINDI WA TATU ZA CECAFA KUCHEZWA NYAYO.
MECHI za kutafuta
mshindi wa tatu na fainali zitachezewa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi
hapo Alhamisi terehe 12 mwezi huu. Aidha mechi mbili za nusu fainali ya Senior
Challenge Cup zitakazochezwa leo, zitaandaliwa kwenye viwanja viwili vya
Kenyatta,mjini Machakos na ile ya Mombasa.Timu ya taifa Harambee Stars itavaana na Kilimanjaro Stars ya Tanzania Machakos majira ya jioni kwa wakati huo Zambia ikitifuana na Sudan huko Mombasa.
Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Sam Nayamweya alithibitisha hayo kufuatia makubaliano na kamati mandalizi ya uwanja huo ambao waliafikiana kutenganisha michuano hiyo miwili kwa faida ya mashabiki.
Awali nusu fainali
zote zilipangiwa kuchezewa katika uwanja wa Moi jijini Kisumu lakini zikafutiliwa
mbali kwa sababu ya kuwa uwanja huo bado upo chini ya ukarabati.
“Baada ya kufanya
mashauriano ya kina na maafisa waandalizi wa dimba hili, tumeamua kwamba uwanja
wa Mombasa utaanda nusu fainali kati ya Zambia na Sudan huku ile ya Kenya na
Tanzania zikiwa Machakos,” Nyamweya akathibitisha.
No comments:
Post a Comment