Tuesday, December 31, 2013

MAPINDUZI CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO JANUARI MOSI
 MAPINDUZI CUP, Kombe la Kusheherekea Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, litaanza kushindaniwa Jumatano Januari Mosi huko Amaan Stadium, Zanzibar na Gombani Stadium, Pemba na Timu 12 zinatarajiwa kushiriki.
Wenyeji Zanzibar wanawakilishwa na Timu 4 ambazo ni KMKM, Chuoni, Spice Stars na Clove Stars.
Tanzania Bara ina Timu 4 ambazo ni Mabingwa Yanga, Simba, Azam na Mbeya City.
Timu kutoka nje ya Tanzania ni 4 nazo ni URA na KCC za Uganda na AFC Leopards na Tusker za Kenya.
Timu hizo zimegawanywa katika Makundi Matatu ya Timu 4 kila moja na Timu mbili za Juu toka kila Kundi pamoja na Timu mbili zitakazomaliza Nafasi ya Tatu Bora zitasonga.
Makundi:
KUNDI A: Mbeya City, Clove Stars (Kombaini ya Pemba), Chuoni, URA (Uganda)
KUNDI B: Simba, KMKM, AFC Leopards (Kenya), KCC (Uganda) 
KUNDI C: Azam, Tusker (Kenya), Yanga, Spice Stars (Kombaini ya Zanzibar)
Katika Mechi za fungua dimba hapo kesho, zitakazochezwa Mjini Zanzibar Uwanja wa Amani, Wenyeji KMKM wataanza na KCC ya Uganda na kufuatiwa Usiku na Mechi kati ya Simba na AFC Leopards ya Kenya.
Mashindano haya yataendelea Alahamisi kwa Mechi nne.
Alhamisi Januari 2
[Amaan Stadium, Zanzibar]
Spice Stars v Azam [Saa 10 Jioni]
Yanga v Tusker [Saa 2 Usiku]
[Gombani Stadium, Pemba]
URA v Chuoni [Saa 8 Mchana]
Mbeya City v Clove Stars [Saa 10 Jioni]

No comments: