HALI YA MICHAEL SCHUMACHER BADO TETE.
FAMILIA ya dereva
nguli wa mashindano ya langalanga, Michael Schumacher imeendelea kuwa pembeni
ya kitanda chake wakati akipigania
maisha yake kufuatia ajali aliyopata wakati akiteleza katika barafu katika
milima ya Ufaransa. Meneja wa dereva huyo Sabine Kehm amesema mkewe
Corinna, binti yake Gina Maria na kijana wake wa kiume Mick bado wameendelea
kubakia katika hospitali ya Grenoble ili kujua hatma ya mpendwa
wao. Schumacher ambaye ambaye ni bingwa wa dunia mara saba wa mashindano
ya langalanga alipata majeraha ya kichwani wakati alipoanguka kwenye tukio
hilo. Mkuu wa hospitali hiyo profesa Jean-Francois Payen amesema nyota
huyo bado ameendelea kubakia katika wodi ya watu wanaohitaji uangalizi maalumu
huku akiwa amepewa dozi nzito za usingizi ili ubongo wake uweze kujitibu
taratibu baada ya upasuaji.
No comments:
Post a Comment