TANZANIA YAPANDA KWA NAFASI TANO VIWANGO VYA FIFA
TANZANIA imekwea kwa nafasi
tano katika viwango vya soka vinavyoandaliwa kila mwezi na Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA. Mwezi uliopita Tanzania ambayo imekuwa ikishuka na kupanda
katika viwango hivyo iliporomoka mpaka nafasi ya 129 lakini katika viwango vilivyotolea
leo imepanda tena mpaka katika nafasi ya 124. Kwa upande wa Afrika Ivory
Coast imeendelea kuongoza kwa kushika nafasi ya 17 katika viwango vya dunia
ikifuatiwa na Ghana waliopo katika nafasi ya 24 huku Algeria wakiwa nafasi ya
tatu kwa kushika namba 26. Wengine ni Nigeria waliopo nafasi ya 36 na tano
bora kwa upande wa Afrika inafungwa na Misri waliokwea kwa nafasi 13 mpaka
nafasi ya 38 katika viwango hivyo.
No comments:
Post a Comment