PLATINI ASEMA SOKA INA NAFASI KUBWA KUPAMBANA NA UBAGUZI
RAIS wa Shirikisho la
Soka baani Ulaya-UEFA Michel Platini amesema katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
kuwa soka lazima liongoze harakati za kupinga ubaguzi wa rangi ndani na nje ya
uwanja. Kutoka na mchezo wa soka kupendwa na mashabiki wengi zaidi dunia, Platini
anadhani mchezo huo utakuwa na nafasi kubwa ya kutokomeza ubaguzi. Platini
amesema kutokana na umaarufu mkubwa uliopo katika soka ndio kuna wajibu wa
kuongoza kampeni hizo.
Katika miaka ya
karibuni, UEFA pamoja na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limeongeza juhudi za
kupambana na ubaguzi wa rangi michezoni na mojawapo ya adhabu zilizoongezwa ni
pamoja na faini ya kiasi kikubwa cha fedha na kucheza katika viwanja vitupu kwa
ajili ya vilabu na timu za taifa ambazo amashabiki wake watakutwa na hatia ya vitendo
hivyo.
No comments:
Post a Comment