DUNGA ATIMULIWA NA TIMU YAKE BAADA YA KUPATA VIPIGO VINNE MFULULIZO
KLABU ya Internacional ya Brazil imemtimua kocha wake
Dunga baada ya kupata kipigo cha nne mfululizo katika Ligi Kuu ya nchi
hiyo. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo ilidai
kulibadilisha benchi zima la ufundi la klabu hiyo akiwemo kocha
mkuu. Klabu hiyo imemteua kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 20 aitwae
Clemer kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa mchakata wa kutafuta kocha mwingine
ukiendelea. Dunga ambaye aliiwezesha timu hiyo kushinda mechi 26 na
kupoteza tisa katika mechi 53 ambazo imecheza, alitimuliwa wakati wakiwa Rio de
Janeiro ambapo walichapwa mabao 3-1 na Vasco da Gama
No comments:
Post a Comment