TAARIFA MUHIMU KUTOKA TFF LEO
KAMATI
ya Uchaguzi imepitisha majina ya waombaji 40 kati ya 58 kwa ajili ya uchaguzi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania (TPL
Board) utakaofanyika mwezi ujao. Waliopitishwa
katika orodha hiyo ya awali kwa upande wa Bodi ya Ligi ni Hamad Yahya Juma
(Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti). Kwa upande wa Kamati ya Uendeshaji
(Management Committee) ni Kazimoto Miraji Muzo na Omar Khatib Mwindadi.
Walioondolewa kwa vile si wenyeviti wa klabu za daraja la kwanza kama kanuni
zinavyotaka ni Michael Njuweni Kaijage, Salum Seif Rupia na Silas Masui
Magunguma. Kanda
namba moja (Kagera na Geita) aliyepitishwa kuwania nafasi ya ujumbe Kamati ya
Utendaji ya TFF ni Kaliro Samson wakati Abdallah Hussein Musa ameondolewa kwa
kutojaza fomu ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.
Jumbe
Oddessa Magati, Mugisha Galibona na Vedastus Lufano wamepitishwa kuwania ujumbe
kupitia Kanda namba mbili (Mara na Mwanza). Samwel Nyalla ameondolewa kwa
kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi wa TFF kwa
kutoonesha malengo yake. Waliopitishwa
katika Kanda namba tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Swain a Mbasha Matutu
wakati Stanslaus Nyongo ameondolewa kwa kukosa sifa ya uongozi wa angalau
uzoefu wa miaka mitano kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF. Kanda namba nne (Arusha na Manyara)
wamepitishwa wote watatu; ambao ni Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii
Ali. Kanda namba tano (Tabora na Kigoma) nao wamepitishwa wote; Ahmed Idd Mgoyi
na Yusuf Hamis Kitumbo. Blassy
Kiondo amepitishwa peke yake kuwania ujumbe Kanda namba sita (Katavi na Rukwa)
huku Ayoub Nyaulingo aliondolewa kwa kutokuwa na uzoefu uliothibitika wa miaka
mitano katika uongozi wa mpira wa miguu. Naye Nazarius Kilungeja, Kamati ilikataa maombi yake ya
kugombea ujumbe kutokana na vitendo vyake visivyo vya kimichezo ambavyo kwa
kiasi kikubwa vilisababisha migogoro kwenye Mkoa wa Rukwa, hivyo suala lake
litawasilishwa kwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi. Kanda namba saba (Iringa na Mbeya)
waliopitishwa ni David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve na Lusekelo Elias
Mwanjala. Cyprian Kuyava hakupitishwa kwa vile hana uzoefu wa uongozi kwa
mujibu wa Katiba ya TFF huku Ayoub Shaib Nyenzi akiondolewa kwa kushindwa
kuthibitisha uraia wake. Elliud
Peter Mvella ameondolewa kwa kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa
Pamoja (collective responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya
Kamati ya Utendaji ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye
muhtasari na baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa. Suala
lake limewasilishwa katika Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi. Waliopitishwa kuwania ujumbe kupitia
Kanda namba nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama na Stanley William
Lugenge wakati Kamanga Tambwe ameondolewa kwa vile alipatikana na hatia ya
kushiriki kwenye tuhumu za rushwa kwa waamuzi na kufungiwa na TFF. Kanda namba tisa (Lindi na Mtwara)
waombaji wote watatu wameptishwa. Waombaji hao ni Athuman Kingome Kambi,
Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder. Pia waombaji wote wa Kanda
namba kumi (Dodoma na Singida), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima na
Charles Komba wamepitishwa. Waombaji
wanne kati ya watano wamepitishwa kwa Kanda namba 11 (Morogoro na Pwani).
Waliopitishwa ni Farid Mbarak, Geofrey Nyange, Juma Abbas Pinto na Twahil Twaha
Njoki. Riziki Juma
Majala ameondolewa kwa vile akiwa mtendaji mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Pwani (COREFA) alishindwa kusimamia Kanuni za Ligi kwa kuruhusu timu
ambayo si mwanachama wa wanachama wa COREFA kucheza ligi, hivyo kusababisha
mgogoro mkubwa kiasi cha mwananchi mmoja kufungua kesi ya kusimamisha Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL). Suala lake litawasilishwa Kamati ya Maadili kwa ajili
ya hatua zaidi. Kanda
namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) wamepitishwa waombaji wote wawili. Waombaji hao
ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed. Waombaji wawili kati ya watano
wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam). Wagombea wawili kati ya watano
wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam). Wagombea
hao ni Alex Crispine Kamuzelya na Muhsin Said Balhabou.
Walioondolewa
ni Omar Isaack Abdulkadir kutokana na vitendo vyake vya kutoheshimu na
kutotekeleza maagizo ya TFF kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF.
Atapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi. Shaffii Kajuna Dauda ameondolewa kwa
kutumia nyaraka ya mawasiliano baina ya FIFA na Rais wa TFF bila idhini na
kuiweka hadharani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, hivyo kukiuka
maadili kwa kumiliki nyaraka ambazo hazikuwa kwenye mamlaka yake. Suala lake
linapelekwa katika Kamati ya Maadili. Naye Wilfred Kidao ameondolewa kwa kutumia nyaraka za
Kamati ya Utendaji ya TFF bila ridhaa ya kamati, hivyo kukosa uadilifu. Suala
lake linawasilishwa kwenye Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi. Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa
Rais, waombaji wote watatu wamepitishwa. Waombaji hao ni Imani Omari Madega,
Ramadhan Omari Nassib na Wallace John Karia. Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal
Emil Malinzi wamepitishwa kuwania nafasi ya Rais. Omari Mussa Nkwaruro ameondolewa
kwa kuwasilisha cheti chenye utata, hivyo kukiuka utashi wa Ibara ya 27(7) ya
Katiba ya TFF. Pia aliwasilisha taarifa za uongo kuhusu uzoefu na kukiuka
Kanuni za Maadili, hivyo suala lake linapelekwa Kamati ya Maadili. Naye Richard Julius Rukambula
ameondolewa kwa hakukidhi matakwa ya kugombea uongozi kwa mujibu wa Ibara ya
12(2)(e) ya Katiba ya TFF inayokataza masuala ya mpira wa miguu kupelekwa
katika mahakama za kawaida. Hivyo naye anapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa
hatua stahiki.
POULSEN ASEMA TAIFA
STARS INATAFUTA NAFASI YA PILI
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
amesema wanaipa umuhimu mkubwa mechi ya mwisho ya mchujo ya Kombe la Dunia
dhidi ya Gambia kwa lengo ni kuhakikisha wanamaliza wakiwa wa pili katika kundi
hilo. Mechi hiyo itachezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul, Gambia
ambapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiem Lager itaondoka kesho
(Septemba 4 mwaka huu) saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia
Dakar, Senegal. Kim amesema wanataka kushinda ugenini, kwani licha ya kuwa
wameshatolewa lakini ushindi utawaongezea pointi kwa ajili ya viwango
(rankings) vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na pia kuepuka
kuanzia ngazi ya awali ya mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
kwa fainali za 2015. “Tunacheza mechi hii tukiwa katika mazingira magumu,
kwani wengi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza ni majeruhi. Sijawahi kukutana na
hali hii tangu nilipoanza kuifundisha Taifa Stars, lakini tumejipanga
kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Kim. Amesema kwa mipango ya timu
yake mechi hiyo ni muhimu tofauti na wengi wanavyofikiria, na uamuzi wake wa
kumwita beki Henry Joseph amezingatia mambo mengi ya kiufundi ikiwemo nafasi
anayocheza na uzoefu wa mchezaji aliyekuwa akicheza nchini Norway katika klabu
ya Kongsvinger IL. Wachezaji majeruhi katika kikosi hicho ni Shomari
Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Salum Abubakar, Athuman Idd na John
Bocco. Vilevile wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu hawatakuwemo
kwenye safari baada ya klabu yao ya TP Mazembe kutuma taarifa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo mchana ikidai ni wagonjwa. Wachezaji
wanaoondoka kwenda Banjul ni Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa, Amri
Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni
Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa,
Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.
IRINGA YAINYANYASA RUVUMA COPA COCA-COLA
Iringa imeanza kwa kishindo michuano ya Copa Coca-Cola kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Septemba 3 mwaka huu) kuitandika Ruvuma mabao 4-0. Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika ya 14 na Justin Luvanda huku Alphonce Kalinga akifunga la pili dakika ya 43. Mabao mengine yalifungwa na Juma Rogani katika dakika ya 49 na Luvanda akafumania tena nyavu dakika ya 59. Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Ruvuma kupoteza ambapo ya kwanza ililala mbele ya wenyeji Mbeya kwa mabao 3-0.
IRINGA YAINYANYASA RUVUMA COPA COCA-COLA
Iringa imeanza kwa kishindo michuano ya Copa Coca-Cola kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Septemba 3 mwaka huu) kuitandika Ruvuma mabao 4-0. Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika ya 14 na Justin Luvanda huku Alphonce Kalinga akifunga la pili dakika ya 43. Mabao mengine yalifungwa na Juma Rogani katika dakika ya 49 na Luvanda akafumania tena nyavu dakika ya 59. Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Ruvuma kupoteza ambapo ya kwanza ililala mbele ya wenyeji Mbeya kwa mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment