MAN UTD YAMALIZA HASIRA KWA LIVERPOOL, YAICHAPA 1-0 KOMBE LA LIGI, SASA KUVAANA NORWICH,ASERNAL KUVAANA NA CHELSEA RAUNDI YA NNE, NEW CASTLE NA MAN CITY

Timu ya Manchester United
imeibamiza timu ya Liverpool bao 1-0 katika mchezo wa kombe la ligi na kufuta
machungu ya kufungwa na Manchester City mabao 4-1 mwishoni mwa wiki katika ligi
kuu nchini ungereza.
Katika mchezo huo macho yote
yalikuwa kwa Luis Suarez baada ya kurejea Liverpool kufuatia kumaliza adhabu
yake ya mechi 10, lakini Javier Hernandez ndiye aliyeiua liverpool kwa bao lake
pekee lililoipeleka Manchester United Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu
kama Capital One.
Hatimaye Suarez alicheza mechi
yake ya kwanza ya msimu mpya baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya
kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic msimu uliopita.
Na wakati mshambuliaji huyo wa
Uruguay alizomewa na mashabiki Uwanja wa Old Trafford, alikuwa ni Chicharito
aliyepoza maumivu ya David Moyes kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa
wapinzani, Manchester City katika Ligi Kuu Jumapili.
Nayo Klabu
ya Arsenal itamenyana na wapinzani wao
katika Jiji la London, Chelsea katika Raundi ya Nne michuano hiyo baada ya
kuitoa West Brom kwa penalti 4-3 Uwanja wa Hawthorns.
Mechi
hiyo ilisha kwa sare ya 1-1 usiku wa leo. Manchester United baada ya kuwatoa
wapinzan wao, Liverpool watamenyana na Norwich nyumbani katika Raundi ya Nne.
Birmingham
iliyowatoa mabingwa watetezi Swansea kwa mabao 3-1 watacheza tena nyumbani
katika 16 Bora, safari hii wakimenyana na timu ya Mark Hughes, Stoke.
Licha ya
kupangiwa wapinzani wagumu, lakini The Blues bado wanapewa nafasi kubwa ya
kutwaa tena taji walilolitwaa mwaka 2011, na United ikiwa timu nyingine
inayopewa nafasi pia baada ya kupangiwa Norwich.
Katika
mechi nyingine, Newcastle itaikaribisha Manchester City Uwanja wa St James Park
baada ya kuwatoa Leeds, wakati Hull wataifuata Tottenham siku kadhaa baada ya
kucheza mechi ya Ligi Kuu, Uwanja wa White Hart Lane.
Timu
isiyo na kocha kwa sasa, Sunderland itamenyana na Southampton, wakati West Ham
watakwedna Kaskazini kumenyana na Burnley.
Fulham
ya Martin Jol itaifuata Leicester kusaka nafasi ya Robo Fainali.
No comments:
Post a Comment