Friday, September 6, 2013

AFUNGWA JELA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO

ISMAIL Mohammed (21) mkazi wa kijiji cha Bondeni, wilayani Kyela, mkoani Mbeya, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka kumi (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali.

Mwendesha mashtaka wa polisi, Sajenti Nicholaus Tibba, aliiambia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai mosi mwaka jana katika eneo la kijiwe cha Amazon chaka, kijiji cha Ndandalo, majira ya saa mbili usiku.
Alisema mshtakiwa anatakiwa kupewa adhabu kali ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya, Joseph Luambano, alimhukumu kijana huyo kutumikia kifungo cha maisha jela ili liwe fundisho kwa wengine, Alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao umethibitisha pasipo shaka kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Baada ya hukumu, kijana huyo aliangua kilio kilichosababisha apoteze fahamu.
Tanzania daima

No comments: