WANAFUNZI SUMBAWANGA WAISHI KWA HOFU YA KUBAKWA.
 |
|
Bweni la wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Bomalang'ombe iliyoko wilayani Kilolo, mkoa wa Iringa. Ukosefu wa mabweni
madhubuti kumekuwa kukichangia vitendo vya kubakwa kwa wanafunzi wa kike
Wanafunzi wa kike katika
shule ya sekondari Mzindakaya kijijini Kaengesa, wameelezea vitendo hatari
wanavyokabiliwa navyo vya kubakwa na kudhalilishwa kijinsia mara kwa mara,
kutokana na kukosa uwezo wa kuishi katika mabweni kwa usalama.
Wakizungumza na mwandishi
katika mahojiano maalumu mwishoni mwa wiki, wanafunzi hao wamedai kuwa wamekuwa
wakiona aibu kuripoti visa vya ubakaji wanavyofanyiwa, kwa uongozi wa
shule na kwa wazazi wao.
“Wengi wetu hatujui hatima yetu kwani tunaishi kwa hofu kubwa hususani
usiku, tunakosa raha licha ya kwamba kila mmoja
wetu amepanga chumba.
“Kutokana na visa vya kubakwa mara kwa mara, tumeamua
kulala chumba kimoja wasichana kati ya watatu
hadi sita,” alisema mmoja wao.
Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, wamekuwa wakiogopa na kuona aibu kutoa
taarifa kwa mamlaka husika, na kubakia kukaa kimya na kujiuguza kwa siri
na hata wakipiga kelele, huwa hawapati msaada.
“Tukipiga kelele, hakuna msaada mpaka kukicha ndipo majirani wanapokuja kutupa
pole huku wakidai kuwa licha ya kusikia tukipiga mayowe ya
kuomba msaada, wanashindwa kutoka nje kwa hofu ya
kushambuliwa na watu hao wasiojulikana,“ alisema mmoja wa wanafunzi
hao kwa masikitiko.
Akizungumza na mwandishi shuleni hapo hivi karibuni, Makamu
Mkuu wa shule hiyo, Agatha Okumu, alikiri kuzungumza na
wanafunzi wa kike wanaoishi katika nyumba za kupanga kijijini,
wakamweleza kuwa kumekuwa na visa vingi vya kubakwa.
“Nyumba walizopanga hazifai kuishi, hazina
usalama kutokana na milango ya vyumba kuwa mibovu na usiku
wanalazimika kuegesha vinu kuzuia isifunguke.
“Sasa imekuwa rahisi kwa ‘wabakaji‘ kusukuma tu milango hiyo na
kuingia ndani na kuwaingilia kimwili na kutokomea
kusikojulikana,“ alisema.
Alisema visa vya kubakwa wanafunzi hao wa
kike ni vingi, lakini vitatu tu ndio vimeripotiwa
hadi sasa ambapo kisa cha kwanza
kiliripotiwa baada ya wanafunzi watatu kubakwa, na
mtuhumiwa alisakwa na kukamatwa na kufikishwa katika vyombo
vya dola.
Kwa mujibu wa Mwalimu Okumu, visa vingine ni pamoja na
mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo,
aliyejiua kwa kunywa sumu ya panya, baada ya
kubakwa yeye na mwenzake mwingine.
Mtu aliyewafanyia hivyo, kwa maelezo ya Mwalimu Okumu, alivamia chumbani mwao
walimokuwa wakiishi watatu na kuwatishia kuwaua iwapo
wangepiga kelele.
“Juzi tu wanafunzi sita waliokuwa wakiishi chumba kimoja wamenusurika
kubakwa na watu wawili waliowavamia usiku wakiwa
wamelala chumbani mwao.
“Hata hivyo walishindwa kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji baada
ya kukuta ni wengi na walianza kupiga mayowe, wakaishia
kuwapora Sh 1,100 walizokuwa nazo, wakawapiga kwa marungu na
kutokomea kusikojulikana,“ alisema Mwalimu Okumu.
Mkuu wa shule hiyo, Nicholas Thomas amewatupia lawama
majirani wanaoishi karibu na nyumba walizopanga wanafunzi
hao, kwa kutowapatia msaada wowote licha ya wao kupiga
mayowe ya kuomba msaada.
Mwalimu Thomas aliwataka wazazi kuchangia gharama za watoto
wao kuishi katika mabweni shuleni hapo, ambapo
kwa mtoto mmoja kwa muhula, mzazi anatakiwa kuchangia
magunia mawili ya mahindi, debe moja la maharage na Sh 40,000
za ujira wa mpishi.
Umasikini wa wazazi wao, umedaiwa kusababisha wanafunzi hao kushindwa kulipia
gharama za kuishi katika mabweni ya shule hiyo, na kwa kuwa wanahitaji elimu,
wakalazimika kupanga nyumba mbovu, ambazo ndizo hufanyiwa vitendo hivyo.
Mwandishi alipotembelea baadhi ya nyumba walizopanga wanafunzi hao na
kushuhudia zikiwa katika hali mbaya, kwani hazina vyoo na wala hazijazungushiwa
uzio kwa ajili ya usalama wao.
“Kama unavyoona choo kilichopo ni kibovu, hakina hata mlango na
kiko nje meta kadhaa kutoka katika nyumba hii. Kutokana na hofu ya kutoka nje
kujisaidia wakati wa usiku, tunalazimika kujisaidia kwenye makopo tunayohifadhi
vyumbani kisha asubuhi tunaenda kumwaga uchafu huo chooni,”
alisema.
Uchunguzi wa mwandishi umebaini kuwa kodi ya pango ya vyumba hivyo ni Sh 1,000
kwa mwezi.
|
No comments:
Post a Comment