WALIOFANYISHA MTOTO NGONO NA MBWA WASHINDWA RUFAA
MAHAKAMA
ya Rufaa imetupilia mbali maombi ya rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa
na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, iliyowatia hatiani Shija
Madata na wenzake wawili kutumikia kifungo cha miaka 55 jela baada ya
kumfanyisha ngono mtoto na mbwa.
Rufaa hiyo
ilitupiliwa mbali na jopo la majaji watatu; Natharia Kimaro, Ibrahimu
Juma wakiongozwa na Jaji Januari Msofe, wakisema hoja za
warufani hazikuwa na mashiko ya kubatilisha hukumu ya awali.
Akisoma
hukumu hiyo jana kwa niaba ya jopo hilo, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani,
Bampikya Willibard, alisema baada ya majaji kupitia hoja za warufani
walibaini hazina mashiko kulingana na kosa walilotenda.
Alisema
kuwa waomba rufaa walitenda kosa baya. Kwamba mbali na kumshushia hadhi
mwathirika wa tukio hilo, kulikuwa na mazingira ya kumsababishia magonjwa.
Alifafanua
kuwa waliamuliwa kulipa kila mmoja fidia ya sh 200,000 na wataendelea kutumikia
kifungo jela kama ilivyoamuliwa na mahakama ya mkoa.
Shija
ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18, kwa pamoja na wenzake
walipatikana na hatia katika kesi ya kumlazimisha mtoto wa miaka 13 kufanya
ngono na mbwa.
Mbali na
Shija, warufani wengine ni Job Mlama, ambaye wakati huo alikuwa na miaka
30 na Anicet Edward, aliyekuwa na miaka 30,
ambao walihukumiwa kifungo cha miaka 40 kila mmoja baada ya
kupatikana na hatia katika kesi hiyo.
Warufani
walihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Gadiel Mariki, baada
ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi na kuwaona walikuwa na
hatia kutokana na shitaka lililokuwa likiwakabili.
Kwamba
kitendo walichokifanya kilikuwa cha kinyama na hakikustahili kuvumiliwa kwenye
jamii iliyostaarabika kama Tanzania, hivyo akatoa adhabu kali ili iwe fundisho
kwa watu wengine.
Shija
anatumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kumrubuni mtoto na
kumpeleka kwenye kambi ya madini ya Barrick kwa nia ya kumfanyisha ngono na
mbwa.
Hakimu
Mariki katika hukumu hiyo alisema katika kosa la pili watuhumiwa Shija,
Job na Anicet watatumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya
kupatikana na hatia ya kumshawishi mtoto kukaa maeneo ya kambini na kumfanyisha
ngono na mbwa.
Kwamba
wote watatu watatumikia jela miaka 20 mingine kwa kosa la kumlazimisha kwa
nguvu mtoto kufanya ngono na mbwa.
Mbali na
adhabu hiyo kwa washtakiwa, Hakimu Mariki aliagiza wamiliki wa mgodi wa Barrick
kumkabidhi mbwa huyo mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza ili amilikiwe
na serikali.
Hata hivyo
alisema kuwa watuhumiwa hao watazitumikia adhabu hizo kwa pamoja, hivyo watakaa
jela miaka 20 kila mmoja na kusisitiza kuwa kama hawakuridhishwa na uamuzi wa
mahakama hiyo wana haki ya kukataa rufaa.
Wakili
Mfawidhi wa Serikali, Edwin Kakoraki, wakati huo, aliiambia mahakama kuwa
tukio hilo lilifanyiika Machi 21, 2008, ambapo watuhumiwa hao walikuwa
kwenye kambi ya utafiti wa madini ya Barrick wilayani Sengerema.
Kwamba walimlazimisha
mlalamikaji ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi
Sota kufanya ngono na mbwa, ambapo siku ya tukio mlalamikaji alikwenda
kwenye kambi hiyo akiwa na Shija ambaye ni rafiki yake baada ya kumfuata
nyumbani kwao saa 1:00 usiku na kumuomba amsindikize kwa rafiki yake wa kiume,
aliyekuwa mshitakiwa namba moja Job Mlama.
Mahakama
ilielezwa kuwa Shija na mlalamikaji walipofika kwa Job, walipewa chakula
na kisha maji ya kuoga, baadaye Shija alijilaza kitandani kwa Job na ilipofika
saa 4:00, Shija na Job walimwambia mlalamikaji waende kwenye chumba kingine
wakazunguke kisha watarudi.
Ilidaiwa
kuwa mlalamikaji alikubaliana na kauli ya rafiki yake, hivyo kuondoka
wote watatu na kuelekea kwenye nyumba ambacho Shija na Job walikuwa wakimpeleka
mbwa na walipofika kwenye banda la mbwa walimkuta Anicet ambaye ni
mwangalizi wa mbwa.
Ilidaiwa
kuwa watuhumiwa wote watatu walishirikiana kumvua mlalamikaji nguo zote na
kumsukumia kwa mbwa dume mwenye rangi nyeusi na Anicet kumuonyesha ishara
mbwa huyo ambaye alianza kumwingilia mlalamikaji.
Kwamba
wakati mbwa huyo ikimwingilia kinyume cha maumbile, mlalamikaji alikuwa akipiga
kelele kuomba msaada lakini washitakiwa wote watatu walikuwa wakicheka na
kushangilia.
Tanzania daima
No comments:
Post a Comment