WAHUDUMU WA HOSPITALI WADAIWA KUFANYA MAPENZI NA WAGONJWA
Watumishi
wawili katika zahanati ya Mwanhala wilayani Nzega, wamekumbwa na kashfa ya
kufanya mapenzi na wagonjwa hospitalini.
Kutokana na kashfa hiyo,
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bitun Msangi, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya
Nzega, kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa watumishi hao.
Agizo la mkuu huyo
limetolewa hivi karibuni, baada ya Diwani wa kata ya Utwigu, Sawaka Shita
kuwalalamikia watumishi hao mbele ya Baraza la Madiwani, kwa kukithiri kufanya mapenzi
na wagonjwa nyakati za kazi, licha ya kuonywa kwa mara kadhaa.
Diwani huyo aliliambia
baraza hilo kuwa vitendo hivyo vina
hatarisha maisha ya
watumishi hao na ya wananchi, hususani waliotembea nao na kutishia
kuvunja ndoa za wananchi.
Alidai kuwa taarifa hizo
za malalamiko, zilishafika katika
ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji, tayari kwa utekelezaji, lakini wananchi wa kata hiyo walitaka
kuifunga zahanati hiyo, baada ya kukithiri vitendo hivyo vya kufanya mapenzi
katika wodi zilizopo.
Aliomba baraza liwahamishe
na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu watumishi hao, ambapo majina yao
yamehifadhiwa kwa usalama wao, huku jitihada za kuwachukulia hatua
zikifanyika.
Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo, Patric Mbozu alisema
suala hilo ni la
hatari na linapaswa kufuatiliwa kwa umakini ili
lipatiwe ufumbuzi
na wananchi waendelee kupatiwa huduma za tiba.
Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri hiyo, Abraham Mdeme alikiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuwa
suala hilo, litafuatiliwa mapema ikiwemo kuwahamisha kwa kufuata taratibu
zilizopo.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega,
Msangi alisema watumishi hao,
wamevunja maadili ya
afya, hususani kufanya ngono katika wodi za zahanati kwa nyakati za kazi.
No comments:
Post a Comment