MUUZA MAZIWA APEWA KICHAPO KWA KUMZINI NG'OMBE NCHINI
![]() |
Mji wa Embu. |
MCHUUZI
wa maziwa mwenye umri wa miaka 50 alipata majeraha mabaya, aliposhambuliwa na
umati wa watu kwa kupatikana akifanya
mapenzi na ng’ombe katika kijiji cha Kabogi eneo la Kathaari, Embu Kaskazini.
Bw
Nyaga Kirianye anadaiwa kufumaniwa na mkulima mmoja katika eneo hilo akimchafua
ng’ombe huyo mwendo wa saa tatu na nusu asubuhi.
Mkulima
huyo alipiga yowe iliyowavutia wanakijiji ambao walimpa kichapo cha mbwa kabla
ya kuokolewa na naibu wa chifu wa eneo hilo.
Wenyeji
walidai ya kuwa mfanyabiashara huyo ana mazoea ya kuwafukuza wake zake na
inadaiwa alimfukuza mke wake wa hivi karibuni, miezi miwili iliyopita.
Bw
Kirianye alijitetea kwa majirani akisema yeye huwa anavutiwa na ng’ombe huyo
kwa vile hana mke.
Alipelekwa
hospitalini kabla ya kufunguliwa mashtaka.
No comments:
Post a Comment