WANAUME WAMZINI PUNDA MPAKA KUFA HUKO NCHINI KENYA
![]() |
Paul Nderitu Kihia akiwa kizimbani Nyeri ambapo alishtakiwa kwa kumchafua kuku Julai 18, kijiji cha Kigwadi, Kaunti ya Nyeri. Aliachiliwa huru kwa dhamana ya Sh100,000. Picha/KNA
|
Baadhi ya wakazi wanasema waliwaona wanaume hao wanne wakimfunga kamba mnyama huyo lakini hawakuwa wakifahamu waliyopanga kutekeleza
Inadaiwa kuwa mipira ya komdomu iliyotumika ilipatikana baadaye eneo ambalo tukio linadaiwa kutekelezwa, ishara kwamba walikuwa wamejiandaa.
Mwakilishi wa Wodi Gitau Njoroge alitaja kitendo hicho kuwa cha kushangaza na cha kishetani na kuwataka polisi waharakishe uchunguzi.
“Wanawake eneo hili wanalalamika kwamba wananyimwa haki zao katika ndoa kutokana na ulevi. Vitendo kama hivi sharti vilaaniwe na wote,” akasema.
Punda huyo anadaiwa kufariki kwa kukabwa koo na kunyimwa hewa.
Kwingineko, mwanamume alishtakiwa mjini Nyeri kwa kumuingilia kuku.
Paul Nderitu Kihia alikanusha shtaka la kumuingilia kuku Julai 18, kijiji cha Kigwadi, Kaunti ya Nyeri na akaachiliwa huru kwa dhamana ya Sh100,000 na mdhamini wa kiasi sawa.
Polisi waliambia Hakimu John Aringo kuwa mshtakiwa alifumaniwa akitenda kitendo hicho na mwanawe wa kiume wa umri wa miaka 10 ambaye alimpasha habari kakake mkubwa na kwa pamoja wakaripoti kisa hicho kwa chifu na mshukiwa akakamatwa.
Kuku huyo anayedaiwa kumilikiwa na mwanawe mkubwa wa mshukiwa alichukuliwa na polisi kama ushahidi lakini akafariki baadaye. Mzoga wake ulikabidhiwa afisa wa matibabu ya mifugo kwa uchunguzi kubaini chanzo cha kifo. Kesi hiyo itasikizwa tena Agosti 20.
SWAHILI HUB
No comments:
Post a Comment