Monday, June 24, 2013

MECHI YA FAINALI YAMALIZIKA BILA KUMPATA MSHINDI, TIMU ZAAMUA KUGAWANA ZAWADI PASU KWA PASU.

San Ciro Stadium Naliendele
Mchezaji wa salasala akifanya vitu vyake

Huyu ni wa Buti Moka na manjonjo yake

Pata shika nguo kuchanika

Sala sala wakilisakama lango Buti Moka
Mashabiki wakishangilia bao wakiingia uwanjani

Mashabiki wakifanya vitu vyao
David Paul akiwa kazini Sanciro Stedium Naliendele

Waamuzi wa mchezo huo David Paul katika


Mashabiki wakivamia uwanja
 

Mgeni rasmi katika fainali hiyo Bi Salma Hamisi diwani wa kata ya Naliendele
 Mechi ya fainali ya kukata na shoka kati wa watani wa jadi timu ya Buti Moka na Salasala zote za Naliendelea mjini mtwara, imeisha bila kupata mshindi baada ya viongozi wa timu zote mbili kukubaliana kugawana zawadi za mshindi wa kwanza na wa pili sawa kwa sawa kutokana na kumalizika kwa sare ya bao 1 - 1.
Mechi hiyo ya kusisimua ambayo ilipigwa jumapili ya jana katika uwanja wa San Ciro huko Naliendele nje kidogo ya mji wa Mtwara, ilimalizika kabla ya wakati kutokana na fujo zilizozuka uwanjani hapo mda mchache baada ya timu ya Salasala kusawazisha bao katika kipindi cha pili cha mchezo likifungwa na Samson Kilimanjaro.

Buti Moka ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza lililopachikwa na Hamisi Malota bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili ambacho kiliaanza kwa kwa timu ya Salasala kulisakama lango la wapinzani wao wakiwa na lengo la kusawazisha, ndipo walipofaniki kupata bao la kusawazisha na kulipuka kwa shamrashamra, shange, vivijo na ndelemo kwa mashabiki wa Salasala.
Baada ya bao hilo mashabiki wa upande mmoja wakaanza kuleta fujo kwa kumwagia mchanga golikipa wa timu pinzani, ndipo upande wa pili ulipanza kulipa kasasi.
Hapo ndipo zogo lilipoanza na mwamuzi wa mchezo huo Davi Paul akasubiri mpaka muda wa kumaliza ulipowadia akamaliza mpira.

Muandaaji wa ligi hiyo San Ciro Cup Muba S. Muba akawaita viongozi wa pande mbili zote mbili kuzungumzia swala hilo ndipo walipokubalina zawadi ya mshindi wa kwanza tsh. 200,000 na ya mshindi wa pili sh. 100,000 kila mmoja apate sh. 150,000 kwa madai kwamba hata wakirudiana katika uwanja mwingine hali itakuwa hivyo kwa vile timu ya salasala haikuwa na imani na muaandaaji wa ligi hiyo Muba s. Muba kwa vile yeye ni mlezi wa butimoka na amepanga matokeo ya kuipa ushindi timu hiyo.

Ligi iliyoanza mwezi uliopita ilishirikisha timu 16 kutoka vijiji mbalimbali vya wilaya ya mtr mjini na vijijini.

No comments: