SIR
ALEX FERGUSON SASA AAMUA KUSTAAFU RASMI
MENEJA
wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson anatarajia kustaafu kuinoa
klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuifundisha kwa kipindi cha
miaka 26 yenye mafanikio makubwa. Ferguson raia wa Scottland mwenye umri
wa miaka 71 ameshinda mataji 38 toka alipochukua mikoba ya Ron Atkinson Novemba
1986, likiwemo taji la Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu. Mataji hayo
yanajumuisha 13 ya ligi, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, matano ya Kombe la FA
na manne ya Kombe la Ligi.
Ferguson amesema
uamuzi huo wa kustaafu ni uamuzi ambao ameufikiria kwa kipindi kirefu na
kujiridhisha kwamba sasa ni muda muafaka wa kufanya hivyo. Kocha huyo
amesema amesema ilikuwa ni muhimu kwake kustaafu huku akiiacha klabu hiyo ikiwa
imara na anaamini amefanya hivyo na anategemea itaendelea kuwa juu kwa kipindi
kirefu kijacho kutokana na damu changa atakazoziacha.
No comments:
Post a Comment