ANASHIKILIWA NA
POLISI KWA KOSA LA KUVILAWITI VITOTO VYA SHULE
![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Charles Kenyela |
JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni
linamshikilia Ahmad Mohamed Sharif (38), mfanyabiashara na mkazi wa
Mwananyamala Msisiri ’A’ Dar es salaam kwa tuhuma za kuwaingilia kinyume cha
maumbile wanafunzi wanne wa darasa la nne wa Shule ya Msingi Misisiri ’A’.
Ahmad amekuwa akiwaingilia kinyume cha
maumbile wanafunzi hao katika kipindi cha mwezi Aprili na Mei mwaka huu kwa
nyakati tofauti.
Kati ya wanafunzi hao, wawili wana umri wa
miaka 10 na wengine wawili wana umri wa miaka 12 na 11 wote wakiwa ni wanafunzi
wa Misisiri A.Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Suzana Orege (35) alisema wanafunzi
hao wamekuwa na mahudhurio mabaya shuleni kwa zaidi ya mwezi mmoja na ndipo walipojaribu
kuwafuatilia kwa karibu ili kubaini sababu za wanafunzi hao kutohudhuria
shuleni.
Suzan alisema ilipofika Mei 9, mwaka huu
walifanikiwa kuwapata wanafunzi watatu (majina yanahifadhiwa) lakini mmoja
alikimbia kusikojulikana na walipowahoji sababu za wao kutohudhuria masomo,
waliwaeleza kuwa huwa wanatoka nyumbani kama kawaida kwa ajili ya kwenda shule,
lakini huishia nyumbani kwa Ahmed.
Alisema walipohojiwa zaidi walisema baada ya
kufika nyumbani kwake huwawekea CD za
ngono na kisha kuwaingilia kinyume cha maumbile na kuwapa maandazi, chapati,
bagia, biskuti na kuwatishia wasiseme kwa mtu yeyote na endapo watasema
atawafanyia kitu kibaya .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,
Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Charles Kenyela amethibitisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo, ambapo alisema alikamatwa Mei 10, mwaka huu na atafikishwa
mahakamani.
Kamanda ametoa onyo kwa watu wengine wenye
tabia chafu kama hiyo kuacha mara moja kabla ya kukumbwa na mkono wa sheria.
No comments:
Post a Comment