Friday, May 31, 2013

MABINTI WAZIDUNDA HADAHARANI WAKIGOMBEA MUME WA MTU



Wasichana wawili, wakazi wa Sinza, Dar es Salaam ambao majina yao hayakupatikana mara moja, wamenaswa wakizichapa laivu wakidaiwa kugombea bwana.
Tukio hilo la kujidhalilisha lilijiri katika baa maarufu ya Corner iliyopo Sinza-Afrikasana, Dar, majira ya asubuhi wakati watu wakiwa kwenye mishemishe za kuwahi kazini.
Katika tukio hilo, mmoja wa mabinti hao alikuwa akilalamika kuwa kuna mwanaume walikubaliana kwenda kuvunja amri ya sita harakaharaka ili awahi kazini lakini akazidiwa ujanja na shosti wake hivyo akataka kukomboa chake na ndipo alipotolewa manundu.

Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa wasichana hao walijikuta wakizichapa kavukavu wakimgombea mwanaume huyo aliyedaiwa kuwa ni mume wa mtu, mwenye ndoa changa.
Katika timbwili hilo lililojaza kadamnasi, wanaume walishuhudia sinema ya bure baada ya mmoja wa wasichana hao kula kipigo kizito na kuvuliwa nguo ambapo alibaki wazi sehemu za makalio.

GPL

No comments: