MWALIMU ATUHUMIWA KUMWAMBUKIZA MWANAFUNZI VVU
![]() |
Kamanda
Wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman
|
Na Gordon Kalulunga, Mbeya
IMEELEZWA
kuwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Vanessa (jina
linahifadhiwa) iliyopo Mkoani Mbeya aliyekuwa na mahusiano ya kingono mwalimu
wake aitwaye John Mapunda na ameambukizwa virusi vya UKIMWI
(VVU).
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka (17) wakati anahusiana kingono na mwalimu
wake alikuwa anajiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka 2012
lakini hakuweza kufanya mtihani huo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, Mwalimu Mapunda alikuwa na uhusiano wa kingono na
mwanafunzi wake tangu mwaka 2011 akiwa kidato cha kwanza katika shule hiyo na
wakati mwingine mwanafunzi huyo alikuwa analala nyumbani
kwa Mwalimu wake huyo kwa siku kadhaa, kama mkewe.
Habari zinaeleza kuwa mwalimu huyo ambaye anafundisha somo la jiografia
alifanikiwa kumtongoza na kumrubuni mwanafunzi huyo tangu akiwa kidato cha
kwanza kwa kumwongezea maksi kila mtihani unapofanyika.
Baada ya wazazi wa mtoto kufuatilia nyendo za mtoto baada ya kupotea kwa siku tatu
mfululizo, wazazi walitoa taarifa Central Polisi Mbeya ambapo Polisi
walianza kufuatilia.
Siku tatu baadaye, mwanafunzi huyo wa kike alirejea nyumbani kwao. Wazazi
walimpeleka Polisi. Alipobanwa, aliwaambia Polisi kuwa ametoka kwa
mwalimu Mapunda na kukiri kufanya naye ngono bila kinga.
Habari za kiuchunguzi zimeeleza kuwa Polisi na wazazi waliamua kwenda kumpima
afya katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ambapo majibu yalionesha kuwa
mwanafunzi huyo alikuwa ameambukizwa VVU.
Uchunguzi umebaini kuwa, jalada la uchunguzi wa polisi lipo chini ya askari
anayefahamika kwa jina la Andrea Mwambembe na askari mwingine aliyefahamika kwa
jina la Mwashiwuya.
Lakini katika hali ya kustaajabisha, inadaiwa askari hao walipokuwa
wakifuatilia sakata hilo kwa kumfuata mwalimu Mapunda kazini kwake, walipofika,
Mkurungenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Shukran Mwasajobe
alimshitua Mwl. Mapunda na kusababisha kutorokea wilayani Chunya.
Siku iliyofuata Shukran anadaiwa kumfuata Afande Justine Kayombe na Afande mwanaume
lakini mwenye simu iliyosajiliwa kwa jina la Judith Juma, ili kumalizazana
na tatizo hilo.
Katika hali ya kushangaza, Shukran baada ya kukutana na askari hao na kuweka
mambo sawa, alionekana akimfokea askari Sponsor Millinga na kwenda
kumlalamikia kuwa anatafuta rushwa kwake.
Taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa mwalimu Mapunda hajakamatwa kwa kosa lolote
na mwanafunzi aliyebakwa ameshindwa kufanya mtihani huku wazazi wakilalamika.
Kwa sasa mwalimu Mapunda, Shukran na Afande Justine Kayombe wanadaiwa kuwa
maswahiba na mara kadhaa wanaonekana wakiwa pamoja katika hoteli ya Moon Dust
iliyopo kata ya Ruanda eneo la Soweto Mkoani Mbeya.
Taarifa kutoka Ofisi za Ukaguzi kanda zinaonyesha kuwa mwalimu huyo amekuwa
na kashfa ya ngono tangu akiwa katika Shule ya Montifot Sekondari iliyopo
Usangu wilayani Mbarali mkoani Mbeya, na alifukuzwa hapo kabla ya mwakza 2008
baada ya kutuhumiwa kosa kama hilo, la kufanya mapenzi na mwanafunzi.
Taarifa kutoka kwenye familia ya mwalimu huyo zinaonyesha kuwa kati
ya mwaka 2007, muda mfupi kabla hajafukuzwa kazi katika Shule ya Montifot,
mwalimu huyo alianza kukorofishana na mkewe katika suala la ufuska na
walipohamia jijini Mbeya, mkewe alimfumania akiwa na mwanafunzi wa kike
ndani na hivyo ndoa yao kuvunjika papo hapo, huku mkewe akirejea nyumbani kwao
mkoani Tanga.
Ili kuzima sakata hilo, Mkurugenzi wa shule hiyo anadaiwa kutaka kumfukuza Mkuu
wa shule hiyo ambaye anaonekana kuhoji mara kadhaa juu ya sakata hilo ili hali
yeye tayari anadhani amelimaliza polisi
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka (17) wakati anahusiana kingono na mwalimu wake alikuwa anajiandaa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka 2012 lakini hakuweza kufanya mtihani huo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, Mwalimu Mapunda alikuwa na uhusiano wa kingono na mwanafunzi wake tangu mwaka 2011 akiwa kidato cha kwanza katika shule hiyo na wakati mwingine mwanafunzi huyo alikuwa analala nyumbani kwa Mwalimu wake huyo kwa siku kadhaa, kama mkewe.
Habari zinaeleza kuwa mwalimu huyo ambaye anafundisha somo la jiografia alifanikiwa kumtongoza na kumrubuni mwanafunzi huyo tangu akiwa kidato cha kwanza kwa kumwongezea maksi kila mtihani unapofanyika.
Baada ya wazazi wa mtoto kufuatilia nyendo za mtoto baada ya kupotea kwa siku tatu mfululizo, wazazi walitoa taarifa Central Polisi Mbeya ambapo Polisi walianza kufuatilia.
Siku tatu baadaye, mwanafunzi huyo wa kike alirejea nyumbani kwao. Wazazi walimpeleka Polisi. Alipobanwa, aliwaambia Polisi kuwa ametoka kwa mwalimu Mapunda na kukiri kufanya naye ngono bila kinga.
Habari za kiuchunguzi zimeeleza kuwa Polisi na wazazi waliamua kwenda kumpima afya katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ambapo majibu yalionesha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ameambukizwa VVU.
Uchunguzi umebaini kuwa, jalada la uchunguzi wa polisi lipo chini ya askari anayefahamika kwa jina la Andrea Mwambembe na askari mwingine aliyefahamika kwa jina la Mwashiwuya.
Lakini katika hali ya kustaajabisha, inadaiwa askari hao walipokuwa wakifuatilia sakata hilo kwa kumfuata mwalimu Mapunda kazini kwake, walipofika, Mkurungenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Shukran Mwasajobe alimshitua Mwl. Mapunda na kusababisha kutorokea wilayani Chunya.
Siku iliyofuata Shukran anadaiwa kumfuata Afande Justine Kayombe na Afande mwanaume lakini mwenye simu iliyosajiliwa kwa jina la Judith Juma, ili kumalizazana na tatizo hilo.
Katika hali ya kushangaza, Shukran baada ya kukutana na askari hao na kuweka mambo sawa, alionekana akimfokea askari Sponsor Millinga na kwenda kumlalamikia kuwa anatafuta rushwa kwake.
Taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa mwalimu Mapunda hajakamatwa kwa kosa lolote na mwanafunzi aliyebakwa ameshindwa kufanya mtihani huku wazazi wakilalamika.
Kwa sasa mwalimu Mapunda, Shukran na Afande Justine Kayombe wanadaiwa kuwa maswahiba na mara kadhaa wanaonekana wakiwa pamoja katika hoteli ya Moon Dust iliyopo kata ya Ruanda eneo la Soweto Mkoani Mbeya.
Taarifa kutoka Ofisi za Ukaguzi kanda zinaonyesha kuwa mwalimu huyo amekuwa na kashfa ya ngono tangu akiwa katika Shule ya Montifot Sekondari iliyopo Usangu wilayani Mbarali mkoani Mbeya, na alifukuzwa hapo kabla ya mwakza 2008 baada ya kutuhumiwa kosa kama hilo, la kufanya mapenzi na mwanafunzi.
Taarifa kutoka kwenye familia ya mwalimu huyo zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2007, muda mfupi kabla hajafukuzwa kazi katika Shule ya Montifot, mwalimu huyo alianza kukorofishana na mkewe katika suala la ufuska na walipohamia jijini Mbeya, mkewe alimfumania akiwa na mwanafunzi wa kike ndani na hivyo ndoa yao kuvunjika papo hapo, huku mkewe akirejea nyumbani kwao mkoani Tanga.
Ili kuzima sakata hilo, Mkurugenzi wa shule hiyo anadaiwa kutaka kumfukuza Mkuu wa shule hiyo ambaye anaonekana kuhoji mara kadhaa juu ya sakata hilo ili hali yeye tayari anadhani amelimaliza polisi
No comments:
Post a Comment