Friday, March 15, 2013

WACHUMBA WAAMUA KUTOFANYA NGONO MPAKA NDOA.


Sean Lowe na Catherine Giudici

Sean Lowe akimvesha pete ya uchumba Catherine Giudici

Wapendanao nyota huko nchini marekani wameushangaza umma kwa kuamua kutojamiana mpaka watakapo funga ndoa hivi karibuni.

Sean Lowe 29 na Catherine Giudici 26 ambao watu hawakutambua kama walikuwa wachumba wameibuka na kuutangazia umma juzi kwamba wanataraji kufunga ndoa hivi karibuni na wanataraji kuwa wataishi maisha mazuri ya ndoa baada ya kuwa mabachela muda mrefu.

Sean Lowe ambaye ni mfanyabishara maarufu huko Texas, akizungumza na jarida moja nchini humo amesema amekuwa akiishi maisha ya upweke kwa muda mrefu na wamekubaliana na mchumba wake Catherine Giudici ambaye ni mwanamitindo maarufu huko Los Angeles kutoshirikiana katoka tendo hilo mapaka pale watakapokuwa pamoja baada ya kufunga ndoa.

No comments: