TFF YAPANGA KUKUTANA NA
SERIKALI KUZUNGUMZIA SAKATA LA KUFUTWA KWA KATIBA YA 2012
 |
Leodgar Tenga |
SAKATA la uchaguzi wa
Shirikisho la Soka nchini-TFF limechukua sura mpya baada ya shirikisho hilo
kuamua kuiangukia serikali kuhusu tamko lake ililotoa hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kikao cha kamati tendaji ya TFF, rais wa shirikisho hilo
Leodgar Tenga amesema marekebisho ya katiba yaliyofanyika yalikuwa ni halali
kwakuwa walifuata taratibu zote zinazofaa. Tenga amesema kabla ya kufanya
chochote walienda kwa msajili na baada ya siku 15 walikabidhiwa fomu na msajili
ya kuendelea na mchatakato wao hivyo kama kuna makosa yalifanyika kwa msajili
haoni kwanini iwaathiri wao.
Amesema sio nia ya TFF
kubishana na waziri ila wanaamini wakati anatoa tamko hilo hakujua ugumu wa
utekelezaji wake na waliomshauri hawakuwa makini kuona madhara yanayoweza
kujitokeza huko mbele.
Kikao hicho pia kimeamua
kutotuma barua Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwaelezea mabadiliko hayo kwa
hofu ya kufungiwa mpaka watakapokaa na waziri kuangalia uwezekano wa kutafuta
suluhu ya suala hilo.
Serikali kupitia
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenera Mukangara iliamua
kuingilia kati sakata hilo kwa kuifuta katiba mpya ya mwaka 2012 iliyokuwa
ikitumika katika uchaguzi huo pamoja na kumsimamisha msajili huku akiliamuru
shirikisho hilo kutumia katiba ya zamani katika mchakato wake wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment