ISSA
HAYATOU ATETEA KITI CHAKE
RAIS wa Shirikisho la Soka Barani
Afrika-CAF, Issa Hayatou amechaguliwa tena bila kupingwa kuendelea kushika
wadhfa huo kwa kipindi cha miaka mingine minne.
Katika uchaguzi huo Danny
Jordaan ambaye alijitengenezea jina kubwa kimataifa baada ya kuandaa michuano
ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010 ameshindwa kwa mara nyingine
kupata nafasi ya ujumbe katika kamati ya utendaji ya CAF. Jordaan alishindwa na
mgombea kutoka Madagascar aliyetumia jina moja la Ahmad katika uchaguzi huo
ikiwa mara ya pili kukosa nafasi hiyo nyeti baada ya mara ya kwanza kugaragazwa
katika mkutano uliofanyika nchini Sudan miaka miwili iliyopita.
Katika mkutano
huo uliofanyika jijini Marrakech nchini Morocco aliyekuwa mjumbe wa kamati ya
utendaji ya Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA Amadou Diakite alichaguliwa kuwa
mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF. Diakite alifungiwa na FIFA kwa miaka
miwili Novemba mwaka 2010 baada ya kutuhumiwa kupokea rushwa katika skendo ya
kununua kura uliozunguka nchi zilizopewa uennyeji wa kuandaa michuano ya Kombe
la Dunia mwaka 2018 na 2022.
Shirikisho hilo linatarajia kufanya mkutano
mwingine nchini Brazil mwaka 2014 lakini kutakuwa hakuna uchaguzi tena mpaka
mwaka 2015.

No comments:
Post a Comment