Wednesday, March 20, 2013

MUME AMKATA MKEWE VIPANDE VIPANDE, AMTOA UTUMBO NA KUMUUA
Marehemu Fatma Shaban akiwa na watoto wake enzi za uhai wake.
Na Haruni Sanchawa, Pwani

Mwanamume mmoja Peter Ndala 23 anasakwa na jeshi la polisi kwa Kwa tuhuma za kumuua mkewewe Fatuma Shabani 24 na kisha kumkata kata vipande na kumtoa utumbo na yeye kutokomea kusikojulikana.

Unyama huo, ulitendeka Machi 7, mwaka huu, eneo la Kidimu ambalo ni mpaka unaoigawa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Habari zilizothibitishwa ni kuwa Fatma na Ndala, walikuwa wakiishi pamoja kama mke na mume, wakapata mtoto mmoja.

Lakini uthibitisho kama wawili hao walifunga ndoa, ila imeelezwa kuwa Fatma na Ndala walitofautiana na kuanza kuishi kila mtu kivyake.

Habari zaidi zinadai kuwa siku ya tukio, Ndala alimtembelea Fatma kwenye sehemu yake ya biashara, alikokuwa anajishughulisha na kazi ya mama lishe.

“Alipofika eneo hilo alipewa chakula na huyo mzazi mwenzie kisha akala. Ilipofika saa 2 usiku, Fatma alifunga biashara yake na kuanza safari yake ya kwenda nyumbani kwao ambako alikuwa anaishi kwa dada yake.

Waliongozana pamoja, lakini wakati wanaelekea nyumbani mazungumzo yao hayakuwa mazuri, hivyo yule mwanaume akachukizwa na kuamua kumfanyia ukatili huo mzazi mwenzake,” kilisema chanzo cha habari hizo:

“Ndala alimkatakata Fatma, mikononi alimkata vipande viwili, akamchoma tumboni, akamtoa utumbo, baada ya hapo akatokomea kusikojulikana.

Fatma alipiga kelele, majirani walikimbia kwenda kumuokoa na wakakuta muuaji ametoweka.”

Fatma kabla ya kufariki dunia, aliwaambia watu waliofika kumwokoa kwamba aliyemtenda unyama huo ni mzazi mwenzake kisha akamtambulisha kwa majina matatu ya Peter Ndala Kasheba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulricha Matei alisema: “Ni kweli tukio hilo lilitokea na tunamsaka muuaji kwa kushirikiana na polisi wa Kinondoni.”

Chanzo: GPL



No comments: