Wednesday, February 20, 2013

MAWAKILI WA PISTORIUS WANA KIBARUA KUISHAWISHI MAHAKAMA KUMPA DHAMANA.


Oscar Pistorius akiingia mahakamani akiwa amejifunika koti
Oscar Pistorius akiwa kizimbani
Kumekuwa na Kibarua kigumu cha mawakili kupata dhamana kwa mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius kutokana na tuhuma za mauaji ya mchumba wake.

Taarifa zinasema kuwa waendesha mashtaka wanataka kuhakikisha kuwa mahakama haimwachilii mwanariadha huyo kwa dhamana.

Mwanariadha huyo ambaye ni mlemavu anakabiliwa na kosa la kupanga mauaji ya mchumba wake, Reeva Steenkamp mnao tarehe 14 mwezi huu.


Jumanne Pistorius aliambia mahakama kuwa alimpiga risasi marehemu Reeva alipokuwa bafuni akidhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake.

Ni siku ya pili ya kesi itakayoamua ikiwa Pistorius atapewa dhamana au la.

Kesi ya mwanariadha huyo kwa kina haitarajiwi kufanyika hivi karibuni.

Bwana Pistorius aliwasili mahakamani hii leo akiwa ndani ya gari la polisi huku akijifunika kichwa chake kwa blanketi.

Kesi ilichelewa kidogo kufuatia msukumano wa waandishi na watu wengine wakijaribu kuingia mahakamani

Hata mwandishi mmoja alipoteza fahamu katika hali hiyo.

Tayari hakimu anayesikiliza kesi hiyo ameiweka kesi yenyewe katika daraja ya sita maana kuwa ni muaji yaliyokuwa yamepangwa.

Sasa kibarua kipo kwa upande wa utetezi ambao unajitahidi kushawishi mahakama kumpa dhamana Pistorius kwa misingi ya yaliyotokea hata akamuua mchumba wake.

Source BBC

No comments: