Friday, February 22, 2013

MPANGAJI MATOKEO YA SOKA AKAMATWA JANA ITALIA


Kijana anayetuhumiwa kuwa ni moja kati ya mhusika wa genge la upangaji matokeo katika ligi mbalimbali barani ulaya amekamatwa jana na maafisa wa kimataifa wa usalama wa italia baada aya kutafutwa tangu December 2011.
Admir Suljic, ambaye ni mchezaji wa zamani amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Malpensa alhamisi ya jana huko italia akitokea singapore.

Kijana huyo raia Slovenian 31 anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na genge la wapangapji matokeo la Singapore na Balkans ambalo limekuwa likichunguzwa na Bet.

Wahusika wa usalama wamesema kuwa kundi hilo linahusika na upangaji wa matokeo ya wa baadhi ya mechi katika ligi ya mabingwa barani ulaya kuanzia msimu wa mwaka 2009-2010 na 2010-2011 na bado kuna ushahidi unaonekana kuwa aliwahi kutembelea katika makao makuu ya timu ya soka ya napoli.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mtuhumiwa huyo wa upangaji matokeo katibu mkuu wa askari wa kimataifa Interpol , Ronald Noble, amesema kukamtwa kwake kulikuwa kwa muhimu sana kwa sababu watu hawaamini kuwa duniani sheria zipo na hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria hata siku moja.

Amesema kuwa anaami ya kuwa mtuhumiwa atatoa ushirikiano wa hari ya juu kuhakiskisha ya kuwa wanajua mambo mengi zaidi kuhusu genge hilo.

Taarifa hizi zinakuja baada a shikirikisho la soka barani ulaya kutoa taarifa ya kuwa jumla ya mechi

380 katika miaka ya 2008 na 2011 ziligubikwa na upangaji wa matokeo . Maafisa wa kimataifa wa Europol katika uchunguzi waliofanya kuwa mhusika ajuliakanae kama Dan Tan ambaye yupo Singapore ni moja kati ya watuhumiwa ambao bado anatafutwa katika sakata hilo.

Chanzo: CNN


No comments: