FIFA YATHIBITISHA TEKNOLOJIA KWENYE MSTARI WA LANGO KUTUMIKA KOMBE LA DUNIA MWAKANI BRAZIL
SHIRIKISHO la soka Ulimwenguni (FIFA), limethibitisha matumizi ya Teknolojia ya Mstari wa Goli wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2014.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, aliwahi kueleza dhamira yake ya kutaka teknolojia hiyo itumike wakati wa michuano hiyo nchini Brazil, hii ikiwa ni miaka 50 tangu bao la utata la Geoff Hurst lilipofungwa mwaka 1966 wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia.
Teknolojia hiyo ilijaribiwa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, Disemba mwaka jana, FIFA sasa hivi wanatarajia kuanza kuitumia katika michuano ya Kombe la Mabara, wakati wa majira ya joto, na wakati wa Kombe la Dunia.
Taarifa ya FIFA imesema: “Baada ya kufanikiwa kwa matumizi wa Teknolojia ya Mstari wa Goli (GLT) wakati wa Kombe la Dunia la Klabu, nchini Japan, Disemba 2012, FIFA imeamua kutumia GLT kwenye Kombe la Mabara nchini Brazil mwaka 2013 na Kombe la Dunia nchini Brazil 2014.
“Madhumumi ya kutumia GLT ni kuwasaidia waamuzi wa mechi na kufunga mfumo huu kwenye viwanja vyote, tunasubiri mafanikio kwenye ufungaji na mazoezi ya uamuzi kabla ya mechi.
“Kukiwa na teknolojia mbalimbali sokoni, FIFA imetangaza tenda leo, tumeweka vitu tunavyovitaka kiufundi kwa ajili ya mashindano mawili ya FIFA yajayo nchini Brazil
Teknolojia za Hawk-Eye na GoalRef zote zimeshapitishwa na FIFA na zinajipanga kupambana kati ya zenyewe kwa zenyewe na kama ikiwezekana dhidi ya teknolojia zingine kupata haki ya Kombe la Dunia.
HawkEye inajumuisha matumizi ya kamera, wakati GoalRef ina mfumo wa kisayansi zaidi, ikijumuisha sehemu ndogo ya sumaku inayowekwa kulizunguka goli na vifaa vya umeme kwenye mpira, huku taarifa ya bao ikisafirishwa kwa sekunde chache mpaka kwenye saa inayovaliwa na mwamuzi.
HAWK-EYE
Huu ni Mfumo wa Kamera, umezalishwa na Kampuni ya Uingereza ya Hawk-Eye, ambayo ilinunuliwa mwaka jana na Kampuni ya Japan ya Sony, ambao tayari wanamfumo unaotumiwa kwenye mchezo wa tenesi na Kriket.
Kamera sita au saba za kurekodi matukio kwa kasi, zinafungwa pande zote za uwanja, kwenye Paa la kiwanja, zinafuatilia uwepo wa mpira na mfumo wa kompyuta unafanya mahesabu na kujua wapi mpira upo uwanjani, na kutuma maseji za umeme kwenye kifaa kama saa ambacho kinavaliwa na mwamuzi uwanjani, pale mpira unapovuka mstari.
Swali pekee juu ya mfumo huu wa Hawk-Eye, ni je, utaweza kufanya kazi kwenye matukio machache sana ambayo mwili wote wa kipa utakuwa umefunika mpira.
FIFA wamesisitiza kwamba picha hizo hazitaonyeshwa kwenye televisheni kubwa za uwanjani, baada ya tukio lolote la utata, huku mwamuzi pekee ndiyo akishituliwa kama mpira umevuka mstari ama la.
GOALREF
Mfumo huu umetengenezwa kwa ushirikiano kati ya Wadenmark na Wajerumani, GoalRef inatumia eneo la sumaku kutambua kama mpira umevuka mstari ama la. Mistari mitatu ya sumaku inawekwa kwenye maungio ya mpira, kati kati ya bladder na nje, na pale mpira ukivuka mstari hizi zinatambuliwa na Vifaa maalumu vya ufahamu ambavyo vinakuwa kwenye miamba ya goli.
Vifaa hivyo vvya fahamu, vinatuma mawimbi ya umeme ambayo yanavurugwa pale mpira utakapo vuka mstari wa goli na kompyuta inatuma ujumbe kwa mwamuzi, kupitia kwenye saa ambayo amevaa ndani ya sekunde moja.
Ufungaji wa mfumo huu siyo wa bei kali sana kama Hawk-Eye lakini bado ni muhimu. Hapa kinachobakia ni masuala ya kujadili na watengenezaji wa mpira kuruhusu uwekwaji wa mstari hiyo ya sumaku kwenye mpira, lakini tayari GoalRef wameshazungumza na watengeneza wa mipira.
“Kampuni za GLT ambazo zitakuwa tayari zitaalikwa wakati wa ukaguzi wa viwanja vya Kombe la Mabara, tukio hilo kwa sasa limepangwa kufanyika kati kati ya Machi, huku uamuzi wa mwisho ukitarajiwa kutolewa mwanzoni mwa Aprili.”
Uamuzi wa FIFA umekuwa kama kioo kwa Ligi Kuu ya England wanaopanga kuitumia teknolojia hiyo kwenye msimu ujao.
Kumekuwa na utata mwingi kuhusiana na ufungaji wa mabao ikiwa pamoja na bao la Frank Lampard dhidi ya Ujermani wakati wa Kombe la Dunia la 2010.
Bodi ya Vyama vya Soka (IFAB), imeshatoa baraka zao kwa teknolojia za Hawk-Eye na GoalRef wakati wa mkutano wao uliofanyika Zurich mwaka jana
Ligi Kuu ya England iliapa kuleta teknolojia hiyo muda mfupi baada ya uamuzi wa IFAB.
Kombe la Dunia la Klabu, lililofanyika Tokyo, ambalo Chelsea walishiriki ilikuwa michuano ya kwanza kutumia teknolojia hiyo.
No comments:
Post a Comment