AFYA YAKO WIKI HII
UGONJWA WA SARATANI NI TISHIO TANZANIA
![]() |
Muhimbili |
WAKATI wiki hii dunia ikiadhimisha Siku ya Saratani, ugonjwa huo nchini umeelezwa kukua kwa kasi, huku waathirika wa tatizo hilo wakiwa ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 25 na 30.
Daktari wa Kitengo cha Patholojia cha Uchunguzi wa Magonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Innocent Mosha alisema kati ya wagonjwa 17 na 20 hugundulika na saratani kila siku katika hospitali hiyo ya taifa.
“Kwa mwaka mzima wagonjwa wanaogundulika na saratani Muhimbili ni zaidi ya 4,000. Hizo ni takwimu za hapa Muhimbili tu, bado kuna Ocean Road, mikoani na hospitali nyingine binafsi. Ni tatizo kubwa,” alisema Dk Mosha.
Dk Mosha alisema kila siku kitengo hicho huchunguza matatizo ya vivimbe mbalimbali na zaidi ya nusu ya vipimo vya wagonjwa 30 hugundulika kuwa saratani.
“Kwa sasa saratani ya ini inaongezeka kwa vijana wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 25 hadi 30, ambapo kwa siku mbili hadi tatu huwa ni za saratani hiyo,” alisema na kuongeza;
“Mara nyingi saratani hii husababishwa na virusi vya ‘Herpetis B’ na husababishwa na mambo mbalimbali ikiwamo mfumo wa maisha.”
Hata hivyo daktari huyo alisema bado chanzo kikubwa cha saratani ya ini kwa vijana hakijabainika.
Dk Mosha alisema inawezekana ongezeko la kesi nyingi za saratani linasababishwa na ukuaji wa teknolojia, ambapo kwa sasa vipimo vya kitaalamu zaidi vipo nchini.
Dk Mosha alisema saratani zinazoongoza zimegawanyika kwa wanawake na wanaume, ambapo saratani ya shingo ya kizazi na matiti zinaongoza kwa kuwaathiri wanawake, wakati saratani ya tezi dume inaua zaidi wanaume wenye umri wa miaka 50 na zaidi.
Alisema saratani nyingine zinazoongezeka ni saratani ya ngozi inayosababishwa na kukaa juani kwa muda mrefu.
Daktari Bingwa wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa wa Muhimbili, Henry Mwakyoma alisema saratani kuu zinazoongoza kwa hapa Tanzania ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi, tezi dume, ngozi, mifupa, tezi kwa watoto na wakubwa, damu, kongosho, ubongo na ini.
Vifo vya saratani
Katika hatua nyingine Shirika la Afya Duniani, (WHO) linaeleza kuwa asilimia 30 ya vifo vinavyotokana na saratani vinasababishwa na mtindo wa maisha ya mwanadamu.
Shirika hilo limetaja tabia hizo kuwa ni pamoja na kutofanya mazoezi, kutokula matunda, unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara.
WHO ilieleza kuwa asilimia 70 ya vifo hivyo hutokea katika nchi zinazoendelea na zile za kipato cha kati.
Aidha, taarifa kutoka katika shirika hilo zinasema kuwa uvutaji wa sigara unachangia asilimia 22 ya vifo vitokanavyo na saratani na asilimia 72 ya saratani ya mapafu.
Imeelezwa kuwa saratani kuu zinazosababisha vifo duniani ni pamoja na ya mapafu, tumbo, kizazi, ini, na ya maziwa.
Pia WHO inaeleza kuwa asilimia 20 ya vifo husababishwa na saratani inayotokana na virusi vya HBV/HCV, Human Pappiloma Virus (HPV)ambavyo husababishwa na ufanyaji wa ngono na hutokea zaidi katika nchi za Jangwa la Sahara.
Vifo vinavyosababishwa na saratani duniani vinahisiwa kufikia milioni 13.1 ifikapo mwaka 2030,ambapo kwa sasa asilimia 21.4 hutokea kila mwaka katika nchi zinazoendelea.
Saratani ya shingo ya uzazi
Saratani ya shingo ya uzazi imetajwa kuwa ni tishio zaidi kwa wanawake duniani,ambapo kati ya vifo 275,000 asilimia 85 husababishwa na saratani hiyo.
WHO inasema, endapo saratani ya shingo ya kizazi haitachukuliwa hatua zaidi, kufikia mwaka 2030 tutapoteza wanawake 430,000 kila mwaka.
Hivi sasa saratani inaongoza kwa kuua zaidi kuliko Ukimwi , malaria na kifua kikuu.
Utafiti na tiba;
Tunda la Stafeli linatibu saratani
Tunda la Stafeli linatibu saratani
TUNDA la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo vya afya, utafiti umebaini.
Utafiti huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani, umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani, tunda hilo pia ni tiba ya matatizo ya msongo na mfadhaiko.
“Maajabu ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa kuangamiza chembehai zenye saratani pasipo kusababisha madhara katika mwili kama zinavyofanya dawa nyingine za ugonjwa huo au mionzi,” imesema sehemu ya utafiti huo uliochapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la Kemia na Madawa la nchini Marekani, mwaka 2010.
Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976.
Katika utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vina uwezo wa kutibu saratani, lakini matokeo ya utafiti huo hayakutangazwa kwa umma kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za saratani.
Inaelezwa kuwa kirutubisho kilichopo katika stafeli kinatumia jina la kibiashara la ‘Triamazon’ na kimepigwa marufuku kutumika nchini Uingereza na Marekani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitiba.
Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini Korea na kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia ulibaini kuwa stafeli lina uwezo wa kuponya saratani ya tumbo.
Utafiti wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa tunda hilo linaweza kulenga seli za saratani tu, bila kushambulia seli muhimu za mwili kama ambavyo tiba ya mionzi ifanyavyo.
Tunda la Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho Annona Muricata, ambacho ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya saratani.
Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja na kutibu saratani, kirutubisho hicho kilichopo katika tunda hilo pia huweza kutibu vimelea, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, matatizo ya mfumo wa fahamu na sukari.
Utafiti huo unaonyesha kuwa kirutubisho kimegwacho katika tunda hilo kinaweza kwa asilimia kubwa kupambana na saratani bila kumuacha mgonjwa na madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupuAidha huweza kuupa mwili kinga na kukupa nguvu bila madhara yasababishwayo na dawa nyingine.
Tangu mwaka 1976, tunda hilo liliendelea kufanyiwa utafiti katika maabara binafsi zaidi ya 20 duniani.
Stafeli nini?
Stafeli ni tunda la chanikiwiti ambalo linastawi zaidi katika ukanda wa kitropiki.
Mti wa tunda hilo ni mfupi wa wastani, Wabrazili wanauita Graviola na Waingereza wanaliita Soursop. Hapa Tanzani stafeli linajulikana kwa jina jingine la topetope.
Kwa Waingereza, tunda hili ni kubwa lenye uchachu wa kati na utamu mwingi. Ndani yake kuna maganda yenye weupe kama sufi na limesheheni juisi.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Tiba (NIMR) Dk Julius Massaga, alisema taasisi yake haijawahi kufanya tafiti ya aina yoyote kuhusu tiba ya saratani.
“Tuna kitengo cha masuala ya tiba na mambo mengine lakini hatujawahi kufanyia utafiti tunda la stafeli wala dawa nyingine yoyote ya saratani,” alisema Dk Massaga
Mtaalamu wa masuala ya tiba za vyakula, Boniphas Sosthenes wa kituo cha Tiba cha Neema, jijini Dar es Salaam, alisema anafahamu uwezo huo wa stafeli kutibu saratani, lakini hajathibitisha kitalaamu.
Daktari aliyewahi kumtibu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Dk Keisy Mtambo alisema taarifa za kuwa stafeli linaweza kutibu saratani anazisikia, lakini hana uhakika.
“Nasema sina hakika kwa sababu satani ina hatua mbalimbali na kwa watu tofauti,” alisema.
Alisema kwa anavyoifahamu saratani, ni vigumu mno kutibika kwa tunda tu, labda kama tunda hilo limefanyiwa kazi za kitabibu zaidi.
“Kuna saratani kwa watoto, wazee na watu wenye VVU, zina utofauti mkubwa na utafiti huo haujaeleza bayana,” anasema
Source; Mwananchi
No comments:
Post a Comment