ZAMBIA YAVULIWA UBINGWA AFCON, NIGERIA, BURKINA FASO ZATINGA HATUA YA MTOANO
Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika, Chipolopolo ya Zambia, leo wametolewa nje ya mashindano hayo baada ya kutoka sare 0-0 na Burkina Faso katika mechi yao ya mwisho ya kundi C.
Burkina Faso ilianza mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya nyota wake Alain Traore kupata jeraha na kuondolewa uwanjani baada ya dakika kumi pekee.
Traore amefunga magoli matatu zikiwemo mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Ethiopia ambayo walishinda kwa magoli manne ya yai.
Dakika chache baadaye Davis Nkausu, wa Zambia vile vile alijeruhiwa na kuondolewa uwanjani na mahala pake kuchukuliwa na Joseph Musonda baadda ya kugongana na mlinda lango wa Burkina Faso.
Kufikia wakati wa mapunziko timu hizo mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ya kutofangana bao lolote.
Katika kipindi cha pili Zambia ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi zao ziligonga mwamba.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikigawamna alama moja kila moja na hivyo Burkina Faso kusonga mbele baada ya kukusanya jumla ya alama tano nayo zambia ikiridhika la alama mbili.
Nigeria imeongoza kundi hilo kwa jumla ya alama tano huku Ethiopia ikivuta mkia na alama moja.
Kabla ya mechi hiyo Zambia ilikuwa na alama mbili na ilihitaji ushindi katika mechi ya leo ili ifuzu kwa raundi ijayo sawa na Nigeria.
Hata hivyo mabingwa hao watetezi watajialaumu baada ya kukoso nafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo.
Collins Mbesuma na Rainford Kalaba hawakuonyesha mchezo mzuri kama ilivyotarajiwa na uamuzi wa kocha mkuu wa kumuacha nje nahodha wa Chipolopolo huenda ukashutumiwa vikali, na mashabiki wa Zambia.
Kesho ni kundi D ambapo Algeria watavaana na Ivory Coast wakati Togo uso kwa uso na tunisia.
No comments:
Post a Comment